Home » » WAHADZABE WATAKA NYAMA YA NYANI NA NGIRI ILI KUTEKELEZA ZOEZI LA SENSA MWAKA HUU

WAHADZABE WATAKA NYAMA YA NYANI NA NGIRI ILI KUTEKELEZA ZOEZI LA SENSA MWAKA HUU





NA
MWANDISHI WETU
 JAMII
ya Wahadzabe nchini wameitaka serikali kuhakikisha kuwa ina wapatia nyama ya nyani
na ngiri Agosti 24 na 25 mwaka huu, kwa ajili ya kujikusanya ili wapate
kutekeleza mpango wa sensa itakayofanyika Agosti 26  kinyume cha hapo
itakuwa ni vigumu kwao kuhesabiwa.

Kiongozi
wa jamii hiyo, Athuman Gwamanda, alisema kupatiwa nyama hiyo kutawafanya siku
hiyo kutulia katika maeneo  maalum na kurahisisha viongozi wanaosimamia
zoezi hilo la kuhesabu watu kuwapata kirahisi na kuwahesabu.
Alisema
iwapo serikali haitawapatia  mahitaji hayo itambuwe kuwa hawatakuwa tayari
kuhesabiwa siku hiyo kwani wataendelea na shughuli zao za ukusanyaji wa matunda
kama kawaida hivyo kufanya zoezi hilo la kuhesabiwa kuwa gumu.
 Gwamanda
alitanabaisha kuwa nyama ya nyani kwa siku hiyo itakuwa na umuhimu kwani imekuwa
ikitumika kuwapatia supu akina mama ambao wamejifungua watoto ambapo nyama ya
ngiri ni maalum kwa matambiko ambayo yanafanyika kila siku katika jamii hiyo.
Alitaja
nyama nyingine kama nyumbu punda kuwa ni kwa ajili matumizi ya chakula cha
kawaida.
Aidha,
alisema jamii hiyo minatambuwa umuhimu wa sensa lakini hata hivyo, kwa upande
mwingine wanaona kama haiwasidii kwani huduma nyingi za kimaendeleo huwa hazi
wakii kirahisi kwa mfano wao hawahitaji hospitali shule wala barabara.
Jamii
hiyo ambayo inakisiwa kufikia idadi ya watu wasiopungua 1700 imekuwa ikiishi
katika mapori ya  vijiji vya Yaeda Chini Mkoani Manyara ambapo wamekuwa
wakiishi katika vikundi vidogo vidogo katika maeneo ya mkoa huo.

Kwa hisani ya Full Shangwe Blog

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa