Home » » LISSU AMPIGA WASSIRA KIJEMBE KUHUSU MWALIMU NYERERE

LISSU AMPIGA WASSIRA KIJEMBE KUHUSU MWALIMU NYERERE

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba,Tundu Lissu.
 
Mjumbe wa Bunge Maalum la Katiba, Tundu Lissu, amempiga kijembe Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wassira, kwamba analitumia vibaya jina la Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere kwa kuwa si muumini wake wa kweli.
Lissu akichangia bungeni mjadala wa rasimu ya katiba sura ya kwanza na ya sita kuhusu jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na muundo wa Muungano, alisema kwamba kuna watu ndani ya CCM wanaolitumia vibaya jina la muasisi wa Taifa hili, Hayati Mwalimu Julius Nyerere wakati sio waumini wake.

"Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna watu wanajifanya wanamfahamu sana Mwalimu Nyerere, lakini ni watu hao hao waliomkimbia wakati wa uhai wake na kujiunga na NCCR-Mageuzi na baada ya Mwalimu kufariki dunia wakarudi CCM," alisema Lissu huku akishangiliwa, lakini bila kuwataja majina.

Hata hivyo, mwanasiasa pekee aliyeondoka CCM na kujiunga na NCCR-Mageuzi ni Wassira ambaye pia alirejea CCM baada ya Mwalimu Nyerere kufariki dunia.

Kijembe cha Lissu kilionekana kumkera Wassira na alipopata nafasi ya kuchangia bungeni baada ya hati ya Muungano kuwasilishwa, alitumia fursa hiyo kumjibu Lissu kwa kumuita kuwa ni wakala wa shetani.
CHANZO: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa