Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
WATAALAMU wa utafiti nchini wameombwa kujikita kwenye utafiti wa
mifugo na kutoa elimu kwa wafugaji ili waboreshe shughuli zao na kuleta
tija kwa kufuga kisasa.
Ombi hilo lilitolewa jana na Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Elaston Mbwilo
wakati wa ufunguzi wa warsha ya mradi wa utafiti wa kilimo kwa kutumia
mbolea wa Africa RISING iliyowashirikisha wakulima na wafugaji wa
Wilaya ya Babati.
Mbwilo alisema wafugaji wengi nchini hawana maisha bora kwa kuwa
mifugo yao haiwasaidii kimaisha katika kujingizia kipato bora kutokana
na kutojua mbinu za ufugaji wa kisasa, hivyo hawana budi kuangaliwa kwa
upana na kupewa kipaumbele katika masuala ya utafiti.
Alisema idadi ya wakulima na wafugaji katika mkoa huo inalingan, na
kwa upande wa wakulima hali zao kimaisha ni nzuri kiasi, huku
akibainisha kwamba wamepiga hatua katika kilimo kwa vile wanapata elimu
ya mara kwa mara kutoka kwa wataalamu.
Kwa upande wake, mtafiti kilimo wa mradi huo, Festo Ngulo, alitaja
maeneo yanayotekelezwa kwenye mradi huo kuwa yanamgusa mfugaji ambayo
ni jinsi ya kuzalisha mazao kwa kuongeza kiwango cha mavuno, matumizi
ya mbolea yenye virutubisho ya minjingu na malisho.
Mradi huo ulianza kipindi cha mavuno mwaka 2012/13 na utafanyika kwa
miaka mitano kwenye wilaya tatu nchini ambazo ni Babati na Kiteto,
Manyara na Kongwa mkoani Dodoma kutokana na hali ya hewa na rutuba za
maeneo hayo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment