Home » » HANANG WALIA GHARAMA ZA VIWANJA

HANANG WALIA GHARAMA ZA VIWANJA

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 
 
WAKAZI wa Hanang mkoa hapa, wamelalamikia ughari wa bei ya viwanja vya makazi na biashara wilayani humo.
Ukubwa wa bei hizo za viwanja, umebainishwa mwishoni mwa wiki na baadhi ya wakazi hao katika kikao chao na  Mkurugenzi wa halmashauri hiyo kilichofanyika ukumbi wa mikutano wilayani humo, lengo likiwa ni kuzungumzia kwa kina mambo mbalimbali yanayohusu maendeleo ya Hanang.
Wakizungumzia mambo hayo ya maendeleo, baadhi ya
wananchi hao, Massi Gidamisi na Peter Yotamu, walisema, miongoni mwa vitu ambavyo ni kichocheo cha maendeleo ni kuwa na nyumba, na kuhoji watapataje maendeleo wakati viwanja vinauzwa ghari.
“Tunashangaa kuona kitu kama hicho…bei ya viwanja kuwa ghari katika maeneo mbalimbali ya mji wa Katesh ambapo kiwanja kimoja tunauziwa kwa milioni 5 hadi 10… kwa namna hiyo hatutaweza kupata maendeleo, kwani siku zote maendeleo ni nyumba,” walisema.
Waliiomba serikali kupitia halmashauri, kuangalia namna ya kuweka bei nyingine za viwanja ili watu wengi waweze kumiliki viwanja.
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri hiyo, Filex Mabula, alisema atafikisha suala hilo katika Baraza
la Madiwani na kwamba bei zitabadilika kama walivyotoa maoni.
Naye Diwani wa Katesh, Peter Lorry (CHADEMA), alikiri ukubwa wa bei hizo na kwamba ni kikwazo kikubwa kwa wapiga kura wake kujipatia maendeleo ya vitu na fedha,
hivyo anaungana na wananchi kuitaka serikali kupunguza bei ya viwanja hivyo ili kila mwana Katesh aweze kumiliki kiwanja
 Chanzo;Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa