Licha
ya uchaguzi wa viongozi wa ngazi za mitaa, vijiji na vitongoji
kakamilika mwezi uliopita, maeneo karibu 500 hayakuchagua viongozi kwa
sababu mbalimbali.
Kufuatia madai hayo NIPASHE iliwasiliana na Mkurugenzi wa Uchaguzi
wa Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi),
Khalist Luhanda,kuufahamu ukweli.
Tamisemi ilikiri kuwa ina taarifa za mitaa, vitongoji na vijiji karibu 500 kukosa viongozi wapya.
Alisema maeneo hayo hayana viongozi wapya baada ya wananchi kukataa
kuwachagua kwa sababu mbalimbali zikiwamo kuishinikiza serikali kuvipa
vitongoji hadhi ya kijiji. Baadhi ya vijiji wananchi walitaka kijiji
kigawanywe na wapo waliotaka
maeneo yao yawe kata ilhali maeneo yenyewe hayakidhi vigezo.”
Alisema wasimamizi wa uchaguzi ambao ni Wakurugenzi wa Halmashauri,
wameelekezwa kuhakikisha ifikapo mwisho wa mwezi huu maeneo yote yawe
yamefanya uchaguzi uliobakizwa viporo.
“Isipokuwa maeneo ambayo hayakufanya uchaguzi kutokana na
waliyokuwa wagombea kufariki na yale ambayo wananchi kwa sababu
mbalimbali waliteketeza kwa moto, nyaraka na vifaa vyote vya uchaguzi,
kwamfano baadhi ya maeneo mkoani Sumbawanga, itachukua muda kidogo
uchaguzi kufanyika,” alieleza Luhanga.
Luhanga alisema katika maeneo hayo, serikali italazimika kufanya
maadalizi ya uchaguzi upya, ikiwa ni pamoja na kuandika upya majina ya
wapiga kura na wagombea.
Kwa mujibu wa maelezo yake, wamebaini kasoro kadhaa zitakazolazimisha uchaguzi huo kurudiwa katika baadhi ya maeneo.
Hadi anatoa taarifa hizo, alisema serikali ilikuwa ikiendelea na
jitihada za kuhimiza wananchi hao kutumia fursa itakayotolewa ya kurudia
uchaguzi, kuchagua viongozi wao vinginevyo waziri mhusika atatumia
mamlaka ya kisheria, kuhakikisha hakuna eneo litakalobaki bila uongozi.
Alibainisha pia kwamba, maeneo yote yaliyokumbwa na sintofahamu
wakati wa kuapisha viongozi waliyopatikana kwa njia halali ya uchaguzi,
kiasi cha kusababisha wananchi kuapisha waliyodai kuwa ndiyo viongozi
wanaowataka pia yatafanya uchaguzi upya
“Kwa mfano wale Wamasai ambao waliapisha kiongozi wao
kimila,watabaki naye lakini serikali haitambui uongozi wa aina hiyo,
hivyo uchaguzi utarudiwa ili kupata anayetambuliwa kisheria,”alieleza
Luhanga.
Alisema maandalizi ya marudio ya uchaguzi huo, yanaendelea na
kwamba wakati wowote baada ya mwisho wa mwezi huu watatoa taarifa,
ikielekeza kitakachotakiwa kufanyika, ili kuhakikisha kila eneo nchini
linapatiwa uongozi wa kiserikali unaoeleweka, kwa mujibu wa sheria.
CHANZO:
NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
KUELEKEA UCHAGUZI 2015: JE UNAPENDA NANI AWE KIONGOZI WAKO? JAZA FOMU HII FUPI HAPA
docs.google.com
docs.google.com
0 comments:
Post a Comment