Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Na Mwandishi Wetu, Katuma Blog tz.
Waandishi
wa habari nchini wametakiwa kuhakikisha hawatangazi matokeo ya uchaguzi
katika vituo mbalimbali vya kupigia Kura bila idhini ya Tume ya Taifa
ya Uchaguzi (NEC).
Aidha,
wametakiwa kutumia nafasi zao kuzuia machafuko kwa kuandika habari kwa
kufuata miiko ya taaluma na fani ya uandishi wa habari na kuwaondoa hofu
wananchi ya kuibuka kwa machafuko kupitia kalamu zao.
Hayo yameelezwa na
Mkurugenzi wa Idara ya Habari (MAELEZO), Assah Mwambene wakati
akizungumza na waandishi wa vyombo vya habari mbalimbali.
Alisema siku zote waandishi
wa habari wanapotumia vibaya kalamu zao kwa kuandika habari za uchochezi
ndio huwa chanzo cha machafuko.
"Tunapaswa kupima kauli za
wanasiasa kabla ya kuzichapisha au kutangaza, tuongozwe n amisingi ya
utaifa katika kila jambo tunalofanya na pia kuwaelimisha wananchi
kufuata sharia wakati wa kupiga kura na kutangaza matokweo," alisema
Mwambene.
Alisema viasharia vya
uvunjifu wa amani ni pamoja na kauli za baadhi ya viongozi wa siasa,
wanaharakati, baadhi ya vyombo vya habari na mitandao ya kijamii, kauli
za baadhi ya watafiti, viongozi wa dini na watabiri.
Aliwata waandishi kutoegemea
upande wowote wa chama au mgombea, kutoa taarifa linganifu sambamba na
kuwasiliana na vyanzo sahihi vya habari kabla ya kutoa habari hizo kwa
jamii.
0 comments:
Post a Comment