Home » » MTU MMOJA AUAWA KATIKA MGOGORO WA MADARAKA KIJIJINI SIMANJIRO

MTU MMOJA AUAWA KATIKA MGOGORO WA MADARAKA KIJIJINI SIMANJIRO


Mgogoro wa kugombea madaraka ya uwenyekiti wa kijiji cha kambi ya chokaa wilayani Simanjiro umeingia katika uvunjifu wa amani baada ya mmoja wa wajumbe wa serikali ya kijiji anayemuunga mkono mgombea aliyependekezwa na CCM Mbiki Ratoi Bwana Yohana Rometi kuuawa kwa kupigwa na vitu vyenye ncha kali na wananchi  wanaodaiwa kuunga mkono upande wa pili.
ITV ilifika katika kijiji cha kambi ya chokaa katika maziko ya mjumbe huyo wa serikali ya kijiji ambaye anatajwa kumunga mkono mgombea mmoja kati ya wanaogombania nafasi hiyo anayedaiwa kuuawa na mashabiki wa upande wapili katika vurugu zilizofanyika kijjijini hapo na kushuhudia watu wenye uzuni na machozi baada ya mwili wa marehemu Yohana Rometi kuwasiri ukitokea hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro.
Akizungumza na ITV kaka wa marehemu Yohana Rometi Bwana John Rometi amesema tukio ilo limewatisha na anashindwa kuamini kuwa watanzania sasa wamefikia hatua ya kutoana uhai kwa ajili ya ushabiki wa kisiasa tena kwa chama kimoja huku akiiomba serikali itende haki na mmoja wa viongozi wa serikali ya kijiji hicho Kiberesa Kunei akiwataka familia ya marehemu kuto lipiza kisasi kwani wameshaikabidhi serikali kuchukua hatua.
Akihubiri katika ibada ya maziko mchungaji kiongozi wa kanisa la KKKT usharika wa nomieuti wilaya ya Simanjiro Nurueli Mbaga amesema watanzania wa leo wamekuwa wabaya kuliko wanyama kwani zuruma uonevu na ukatili vimeshika nafasi kuliko haki huku mwenyekiti aliyepitishwa na CCM anayedaiwa kuungwa mkono na marehemu ambaye ameapishwa tarehe 29 mwezi decemba mwaka jana Mbuki Molel Ratoi akiwasii wananchi kuacha visasi kwakuwa havina nafasi kwa sasa.
Chanzo:ITV Tanzania

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa