Mbunge wa Simanjiro, Christopher Ole Sendeka.
Akitoa pongezi kwa kamanda huyo ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Graceland Hotel, Mbunge wa Jimbo la Simanjiro, Christopher Ole Sendeka, alisema kuwa uzalendo aliounyesha unapaswa kuigwa na wakazi wengine wilaya humo.
“Chanda chema hivishwa pete,” alisema na kuongeza, “Materi amekuwa mwana Simanjiro wa kwanza ambaye amejinyima pamoja na familia yake…
huyu ni kijana wa kwanza aliyeingia mfukoni mwake na kufumia fedha zake kuwambuka wadogo zake kwa kuwajengea madarasa haya.”
Aliwaomba wana Simanjiro wengine wenye utajiri wa mifugo na madini kutumia sehemu ya mapato yao kuendeleza jamii walikotoka.
Akizungumzia uamuzi wake wa kujenga madarasa hayo, Kamanda Materi, alisema aliguswa baada ya kupita shuleni hapo mara nyingi na kuona wanafunzi walivyokuwa wakiteseka kwa kusoma chini ya miti.
“Niliona sababu ya kufanya kitu fulani kwa watoto wetu…kazi hii nilianza na Mungu na nimemaliza na Mungu na baba yangu alisema aliniambia hii kazi ni ya Mungu na kuisaidia jamii yako na serikali.
“Pale Mungu amebariki kidogo tutaendelea kusaidia,” alisema na kuwahimiza wengine kutosahau kuleta maendeleo maeneo walikotoka.
Sherehe za uzinduzi wa madarasa hayo ulifanyika pia kwa harambee ya kutunisha mfuko wa kukamilisha ujenzi wa shule hiyo ambayo sasa ina madarasa matano.
Katika harambee hiyo Materi na marafiki zake walichanga Sh. milioni 6 wakati Mbunge Sendeka na marafiki zake Sh. milioni 8.
Makundi mbalimbali yakiwemo wazazi wa watoto wanaosoma shuleni hapo walichanga mifugo, fedha taslimu wakiungwa mkono pia na wageni waalikwa.
Jumla ya Sh. milioni 18 .3 zilipatikana zikiwamo fedha taslim na ahadi, bati 20, ng’ombe 42 na mbuzi 36.
Mapema katika risala iliyosomwa na Mwalimu Mkuu wa shule hiyo, Martin Laizer, alisema shule yao ina upungufu wa vyumba vinne vya madarasa, nyumba tano za walimu, madawati, meza, viti na kabati.
Pia inakabiliwa na uhaba wa walimu, vifaa vya michezo, ukosefu wa stoo ya kuhifadhia vifaa, choo cha walimu na wanafunzi, bwalo na maktaba. CHANZO: NIPASHE
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment