Ni Baadhi ya vikundi vilivyopatiwa mikopo yenye thamani ya
shilingi milioni ishirini na kuhimizwa juu ya kurejesha mikopo hiyo kwa
mujibu wa taratibu zilizowekwa ili vikundi vingine navyo viweze kupatiwa
mikopo hiyo.
Ni Afisa Maendeleo ya jamii wilaya ya Hanang,Doris
Nhomange(wa kwanza kulia) akizungumza na vikundi vilivyonufaika na
mikopo hiyo na kuwashauri kwamba wakazitumie fedha hizo kwa madhumuni
waliyoombea.
Ni Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,George Bajuta
(wa pili kutoka kulia) akiongoza mkutano wa kawaida wa Baraza la
madiwani wa Halmashauri ya Hanang,uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano
wa Halmashauri hiyo.
Ni Mkuu wa wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Sara Msafiri
akizungumza na madiwani wa Halmashauri ya Hanang na kusisitiza juu ya
umuhimu wa kuhifadhi misitu pamoja na kuvilinda vyanzo vya maji kwenye
maeneo yao.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Na,Jumbe Ismailly HANANG Machi,01,2018 Mikopo
HALMASHAURI
ya Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara imekabidhi vikundi 16 vya
wanawake,vijana pamoja na walemavu hundi ya mfano yenye thamani ya
shilingi milioni ishirini ili viweze kukuza mitaji,kuboresha maisha na
kuongeza uzalishaji kwenye baadhi ya viwanda vidogo walivyoanzisha.
Akikabidhi
hundi hiyo,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,George Bajuta
alisema vikundi hivyo vimefanikiwa kupata fedha hizo baada ya kukidhi
vigezo vilivyowekwa kati ya vikundi zaidi ya 1,000 vilivyopo katika
wilaya hiyo.
Hata
hivyo Bajuta hakusita kuvisisitiza vikundi hivyo kuhusu umuhimu wa
kurejesha fedha hizo walizokopeshwa kwani utaratibu huo ni wa mzunguko
ili na vikundi vingine navyo viwezo kunufaika na mpango huo.
Naye
Afisa Maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Doris
Nhomange alivitaja vikundi vya wananwake vilivyonufaika na mikopo hiyo
na kata zikiwa kwenye mabano kuwa ni pamoja na Kikundi cha
Amani(Simbay),Tegemeo(Kateshi),Juhudi(Nangwa),Amani(Dawali),Waida
(Mogitu),Kumekucha (Garawa),Kilimo (Endasiwold),Uvumilivu
(Dumbeta),Uyanjo (Getanuwasi na Semeni(Measkroni).
Kwa
upande wa vikundi vya vijana ni Eforti kutoka Kateshi,Daraja Production
kutoka Darajani Jorodomu,Kikundi cha walemavu Ambianse kutoka
Ganana,Ambianse kutoka Ganana,Vijana na kazi kutoka Basotughani na
Mkombozi kutoka Basotughani
Mwenyekiti
wa Umoja wa mafundi Kateshi,Mohamedi Yusufu Mashaka pamoja na
kuishukuru Halmashauri kwa mikopo hiyo,lakini hata hivyo alitumia fursa
hiyo kuwahamasisha vijana wa wilaya ya Hanang kuunda vikundi,wavisajili
na kisha ndipo waombe mikopo.
Katika
hatua nyingine Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu aliweka bayana
kuwa katika mkutano wa Lac Dodoma na katika kikao hicho ilibainika
kwamba Hanang ilikuwa ikidaiwa zaidi ya shilingi milioni mia tatu
walizokuwa wamelimbikiza utoaji huo wa mikopo ya wananwake na vijana.
“Sasa
leo mnatoa shilingi milioni ishirini tunaomba tujue hizo zilizobaki
zinatolewa lini watu wanataka kuwa na mitaji jamani ili muweze kupata
kodi zaidi na ushuru zaidi.”alihoji Dk Nagu.
Kwa
mujibu wa Mbunge huyo suala hilo liliongelewa kwa umuhimu mkubwa na
kwamba wajumbe wa mkutano huo waliazimia fedha hizo zitolewe katika
kipindi kisichozidi miezi miwili na kuomba kupatiwa majibu ni lini fedha
hizo zitapatikana ili wananchi waweze kunufaika nazo.
Akijibu
hoja ya Mbunge Dk.Mary Nagu,Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya
Hanang,George Bajuta licha ya kutokanusha hoja hiyo lakini alijibu
kwamba waliohusika kula fedha hizo ambao hata mbunge huyo anawajua mpaka sasa bado hawajawarudishia.
“Unajua
aliyetafuna ni nani,aliyelimbikiza ni nani na hawatajaturudishia mpaka
leo na hata Tanzania bado inadaiwa na hawajalipa madeni yao sisi
tunaanzia pale tuliposhikilia tunakwenda mbele,tusiangalie nyuma
utageuka kuwa jiwe,na hata wabunge wahoji namna gani mkono unajikuna
pale unapoishia”alisisitiza Mwenyekiti wa Halmashauri.
0 comments:
Post a Comment