Home » » MBUNGE HHAYUMA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI BASSOTUGHANG

MBUNGE HHAYUMA AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA MAJI BASSOTUGHANG

Na Mwandishi wetu, Hanang'

MBUNGE wa Jimbo la Hanang' Mkoani Manyara, mhandisi Samwel Hhayuma Xaday
 ameweka jiwe la msingi la mradi wa maji wa Bassotughang utakaonufaisha watu 
4,995 wa kata ya Hidet.

Watu hao watanufaika kupitia mradi huo wa maji kutoka ziwa
 Bossoutghang baada ya kujengwa kwa mitambo ya kusafisha
 maji hayo na kuanza kutumika kwa matumizi ya binadamu
 hivyo kupunguza changamoto ya upatikanaji wa maji

Mhandisi Hhayuma ameipongeza Serikali ya awamu ya sita 
kwa kuwakumbuka wananchi wa eneo hilo kwa kuwawekea
 miundombinu bora ya upatikanaji wa maji.




0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa