Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi) mhandisi
Joseph Nyamhanga (katikati) akizungumza na viongozi wa wakala wa
barabara nchini (Tanroads) Mkoa wa Manyara, alipotembelea eneo la mji
mdogo wa Mirerani, (kushoto) ni meneja wa Tanroads Mkoani Manyara,
mhandisi Bashiri Rwesingisa
Meneja
wa Tanroads Mkoa wa Manyara, mhandisi Bashiri Rwesingisa (aliyevaa
shati la maua) akimwelezea Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano (Ujenzi) Joseph Nyamhanga (kushoto kwake) juu ya barabara ya
lami ya Kia - Mirerani, ambayo imemalizika inasubiri kufunguliwa.
Barabara
ya lami ya Kia-Mirerani Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, ambayo
imeshakabidhiwa kwa Serikali, inaendelea kuwa kwenye kipindi cha
matazamio kwa muda wa mwaka mmoja.
Mradi
huo wa barabara uliokabidhiwa serikali Mei 31 mwaka huu, mkandarasi
wake anaendelea na kazi ndogo ndogo za ujenzi wa mifereji ya maji ya
mvua, vivuko na vituo vya basi hasa eneo la Kairo.
Meneja
wa wakala wa barabara nchini (Tanroads) mkoa wa Manyara, mhandisi
Bashiri Rwesingisa aliyasema hayo wakati akisoma taarifa ya mradi huo
kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Ujenzi)
mhandisi Joseph Nyamhanga alipotembelea eneo hilo.
Mhandisi
Rwesingisa alisema barabara hiyo yenye urefu wa kilometa 27 iliyojengwa
na kampuni ya China Henan International Cooperation Group (Chico) kwa
gharama ya sh32.2 milioni, chini ya usimamizi wa ujenzi mhandisi mshauri
M/s LEA International Ltd ya India kwa ushirikiano na kampuni ya DOCH
Tanzania Ltd.
Alisema
kazi zilizotekelezwa ni ujenzi wa kiwango cha lami urefu wa kilometa 27
ikijumuisha Kia hadi Mirerani, Mirerani hadi eneo la uwekezaji la
(EPZ), barabara ielekeayo Arusha inayopitia Mbuguni, barabara ya kuingia
na kutoka kituo cha mabasi Mirerani na mzunguko kiwanda cha
TanzaniteOne.
"Ujenzi
wa barabara hii umehusisha pia kujenga mifereji ya pembezoni mwa
barabara kwenye maeneo ya mji, sehemu za kuvuka mifugo na sehemu za
kuvushia huduma muhimu kama waya za simu na umeme," alisema mhandisi
Rwesingisa.
Alisema
mradi huo umekuwa na changamoto za migomo ya wafanyakazi, wananchi
kugoma kuondoa mali zao ndani ya hifadhi ya barabara.
Alisema
mipango ya baadaye ni kujenga kilometa 114 barabara kwa kiwango cha
lami itakayounganisha eneo la EPZ na mji mdogo wa Orkesumet, makao makuu
ya wilaya ya Simanjiro, kama ilivyoainishwa kwenye ilani ya uchaguzi ya
CCM ya mwaka 2015.
Akizungumza
baada ya kukagua mradi huo, Katibu Mkuu wa Wizara hiyo anayeshughulikia
ujenzi, mhandisi Joseph Nyamhanga alipongeza jitihada zilizofanyika kwa
pande zote hadi barabara hiyo ikamalizika.
Mhandisi
Nyamhanga alisema wakati wanasubiri barabara hiyo kuzinduliwa wakati
inaendelea kutumika, watumiaji wanapaswa kufuata masharti ya matumizi ya
barabara hiyo ili waitunze.
Aliitaka
jamii ya eneo hilo ambao kwa muda mrefu walikuwa wanalilia
utengenezwaji wa barabara na ndiyo wanufaika wa mradi huo, kuutunza
vizuri kwani ni kwa ajili ya faida yao na vizazi vijavyo.
0 comments:
Post a Comment