Wananchi
wa Kijiji cha Langai, Wilaya ya Simanjiro mkoani Manyara wamemgomea
Mkuu wa wilaya hiyo, Zephania Chaula kugawa ardhi yao wanayodai
kuimiliki kihalali.
Wakizungumza
katika mkutano wa hadhara jana Machi 18, 2018, wananchi hao
wanaojishughulisha na kilimo na ufigaji wamesema hatua hiyo ya mkuu wa
wilaya ni ubaguzi.
Mmoja
wa wananchi hao, Paulo Simtek amesema wafugaji wamekuwa wakiishi eneo
hilo kwa muda mrefu, lakini kitendo cha mkuu wa wilaya kuchukua mashamba
yao, kuyamega na kuwapatia wakulima kunaweza kuibua migogoro.
Mwenyekiti
wa Kijiji cha Langai, Mathayo Ole Silongoi amesema kuwa sintofahamu
hiyo inatokana na wa uongozi wa wilaya kudharau Serikali ya kijiji na
kufanya uamuzi usiowahusu kwani mashamba hayo yako chini ya Serikali ya
kijiji.
Akizungumzia
suala hilo, Chaula amesema uongozi wa kijiji hicho umekuwa na ubaguzi
wa jamii na ndicho chanzo cha migogoro na kwamba, Serikali itachukua
hatua za kisheria dhidi yao ikiwemo kutoitisha mikutano ya kijiji tangu
walipochaguliwa.
"Huo
uongozi wa kijiji hatua za kisheria zinawafuata kwa kukiuka ya uongozi
wao waache kusema nimegawa ardhi, bali waseme wao wamefanya nini
ikiwemo kuitisha mikutano kusikiliza kero za wananchi na kusoma mapato
na matumizi zaidi wanayoyafanya ni kuendekeza ubaguzi wa ukabila,"
amesema Chaula
Mwenyekiti
wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro, Jakson Siptek amesema wameanza
kuchukua hatua za utatuzi na kuwataka wananchi kuwa watulivu wakati
hatua zinaendelea.
Chanzo: Mwananchi
0 comments:
Post a Comment