Katibu wa CCM Wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Teddy
Athumani(wa kwanza kutoka kulia)akipitia makabrasha ya mkutano wa baraza
la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang kujiridhisha namna
watendaji wa Halmashauri wanavyotekeleza ilani ya chama tawala.
Mbunge wa jimbo la Hanang,Mkoani Manyara,Dk.Mary Nagu (wa pili kutoka kulia) akipitia taarifa ya utoaji mikopo kwa vikundi vya wanawake,vijana na walemavu iliyowasilishwa kwenye mkutano huo na kisha kutaka kufahami shilingi milioni 300 zilizoagizwa kwenye mkutano wa LAC Dodoma zitalipwa lini ili vikundi vya wanawake,vijana na walemavu viweze kunufaika na kujiongezea mitaji yao.
Mkuu wa wilaya ya Hanang,Sara Msafiri akisisitiza jambo kwenye mkutano wa baraza la madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Hanang uliofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo.

Katibu wa vikao vya Halmashauri ya wilaya ya Hanang,Stevine
Yonah(wa kwanza kutoka kushoto) akinukuu maazimio yote ya mkutano wa
Baraza hilo ili watendaji waweze kutekeleza kikamilifu maazimio
hayo.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)
Na,Jumbe Ismailly HANANG Machi,01,2018 Mazingir
KUTOKANA
na hali ya uharibifu wa misitu katika wilaya ya Hanang kuwa kubwa
sana,Mkuu wa wilaya ya Hanang,Mkoani Manyara,Sara Msafiri ameziagiza
kamati za maendeleo za kata kujenga utamaduni wa kujadili katika vikao
vyao juu ya hali ya uhifadhi wa misitu katika maeneo yao.
Akitoa
agizo hilo kwenye mkutano wa kawaida wa Baraza la kawaida la madiwani
wa Halmashauri hiyo,Mkuu wa wilaya huyo aliyataja baadhi ya maeneo ya
vijiji vya Lalaji.Balangida na maeneo mengine hali ya mazingira ni mbaya
sana.
“Kwa
hiyo niwaombe kwamba kamati za maendeleo za kata mjadili na hali ya
hifadhi ya misitu na ninazo taarifa za kutosha na nimejirisha wapo
viongozi wengine ni wa kisiasa wanashiriki katika biashara ya kukata miti,kuchoma na kuuza mkaa.”alisisitiza Mkuu huyo wa wilaya.
Kwa
mujibu wa Mkuu wa wilaya kupitia serikali kuu wameshatoa maagizo kwa
watendaji kwamba mtu yeyote tule atakayetaka kukata miti hata kama
aliupanda mwenyewe ni lazima apate kibali kutoka kwa Mkuu wa wilaya.
Hata
hivyo Sara alisisitiza kwamba ni ukweli usiopingika na alioufanyia
uchunguzi wa kina na kujiridhisha kuwa kuna baadhi ya viongozi wa
kisiasa,wakiwemo madiwani,wenyeviti wa vijiji,vitongoji na watendaji
wanajihusisha na biashara ya kukata micti kuchoma mkaa na kuuza mazao
hayo.
Akimpongeza
Mkuu huyo wa wilaya,Mbunge wa jimbo la Hanang,Dk.Mary Nagu pamoja na
kumpongeza Mkuu wa wilaya kwa jitihada zake za kulinda naa kuhifadhi
mazingira,lakini aliweka bayana kuwa kama kuna jambo ambalo haliendi
vizzuri katika wilaya hiyo ni suala la mazingira.
Diwani
wa kata ya Hanang,mjini Peter Lori alionyesha kutoridhishwa na namna
Halmashauri isivyoujali msitu wa hifadhi wa Mreru kwani kwa kipindi
kirefu serikali imeitelekeza hifadhi hiyo.
Hata
hivyo diwani huyo alifafanua pia kwamba inasemekana hifadhi hiyo ni
mapito ya wanyama na kuhoji kwamba ni lini Mkuu wa wilaya hiyo
atafikiria msitu wa hifadhi Mreru utakuwa hifadhi ya Halmashauri ya wilaya hiyo.
0 comments:
Post a Comment