Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MATUKIO KATIKA PICHA:
WANANCHI WAKIWA KATIKA ENEO AMBALO LINASADIKIWA KUWA NA DHAHABU.
WANANCHI WAKICHUNGULIA SHIMO AMBALO INASEMAKANA NDILO LENYE DHAHABU.
WANANCHI WAKIENDELEA KUCHIMBA MCHANGA KATIKA ENEO LA SHUNU MJINI KAHAMA.
KINA MAMA,VIJANA,WAZEE NA WATOTO WAKIZOA MCHANGA NA KUCHIMBA UDONGO KATIKA ENEO HILO.
MZEE AMBAYE HAKUFAHAMIKA JINA LAKE AKIWA NA VIFURUSHI VYA MCHANGA BAADA YA KUCHIMBA KATIKA ENEO HILO.
WANANCHI WAKIZIDI KUMIMINIKA KUJITAFUTIA RIDHIKI KATIKA ENEO HILO.
AFISA WA JESHI LA POLISI AKIWAZUIA WANANCHI KUINGIA KATIKA ENEO HILO JANA.
WANANCHI WAKIMSIKILIZA KWA MAKINI AFISA WA JESHI LA POLISI KUHUSU KUTOINGIA KATIKA ENEO HILO
SERIKALI wilayani Kahama mkoani Shinyanga
imepiga marufuku uchimbaji wa madini katika eneo la Shunu kata ya Nyahanga
wilayani humo kufuatia kuibuka kwa tetesi jana kuwa eneo hilo lina madini ya
dhahabu.
Hayo yamebainishwa leo na mkuu wa wilaya ya Kahama Fadhil
Nkulu wakati akiongea na Kahama Fm kuhusu hatua waliofikia kufuatia wananchi
kuingia katika eneo hilo na kuanza kuchimba dhahabu pasipo kuwa na kibali.
Nkulu amesema kuwa hakuna ruhusa kwa mtu yeyote kuchimba dhahabu katika eneo hilo
na ameliagiza jeshi la Polisi kumkamata yeyote atakayepatikana anafanya
shughuli za uchimbaji katika eneo hilo.
Sambamba na hayo Nkulu ameongeza kuwa uchimbaji wa madini una
sheria zake hivyo kama mtu anataka kuchimba akate kibali katika ofisi za madini
na afuate taratibu zote ikiwa ni pamoja na kuwahamisha wakazi wa maeneo hayo na
kuwalipa fidia.
Kwa upande wake diwani wa kata ya Nyahanga Maiko Magile
amesema kuwa siku ya leo watu siyo wengi kama ilivyokuwa jana na kwamba
wanaanza kupungua kutokana na kukosa dhahabu.
Magile ameongeza kuwa kwa sasa kuna uharibifu na uchafuzi mkubwa
wa mazingira uliosababishwa na uchimbaji wa Mashimo sambamba na watu kujisaidia
ovyo katika eneo hilo kutokana na kutokuwa na vyoo.
Chanzo Kijukuu
0 comments:
Post a Comment