Home » » WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU WAEPUKE KUJIINGIZA KWENYE SIASA

WANAHARAKATI WA HAKI ZA BINADAMU WAEPUKE KUJIINGIZA KWENYE SIASA


Na Anthony Mayunga-Serengeti

ILI kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia unapungua wilayani Serengeti wasaidizi wa kisheria na Haki za Binadamu wanatakiwa kujikita zaidi kutoa elimu kwa jamii inayoweza badili mitizamo, wakijiepusha kujihusisha na siasa za uchochezi.

Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu (Washehabise) toka 2007 wanatoa huduma ya ushauri kwa wananchi ikiwemo utoaji wa mafunzo ya sheria mbalimbali hususan ya ardhi ili kupunguza migogoro inayopelekea uvunjifu wa amani.

Akifungua mafunzo ya siku tatu kwa yanayoendeshwa na Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kuhusu kuwajengea uwezo masuala mbali mbali ikiwemo katiba ya jamhuri ya Muungano ya mwaka 1977 kwenye ukumbi wa Jamii katibu tawala wa wilaya  Magohu Zonzo aliwataka kuhakikisha wanapanua mtandao ili kusaidia mabadiliko ya mitizamo ya jamii.

“Kazi inayofanywa na Wasaidizi wa Kisheria na Haki za Binadamu inatusaidia sana sisi kama serikali maana wilaya hii migogoro ya ukiukwaji haki ni mkubwa hasa masuala ya ardhi,ili muweze kufanya hayo ni vema mkatanuka mkawa na mtandao kila kata”alisema.

Alisema kuwa wanawake ndio hasa wanakumbwa na mfumo huo kandamizi ambao unawafanya hata kutosema wanapotendewa ukatili  kwa kuwa wamelelewa kuwa watiifu hata kwa maonevu ,hivyo naamini kama shirika litafanya kazi kwa kufuata malengo yake mapinduzi ya uelewa utakuwa mkubwa.

“Kuna tatizo kwa baadhi ya wasiokuwa na maadili mazuri kutumia nafasi hiyo kudanganya wananchi na kujipatia fedha na mwisho kusababisha vurugu,serikali haitasita kuwachukulia hatua wale watakaobainika”alibainisha.

Aliahidi kuwa ofisi ya mkuu wa wilaya itatoa ushirikiano mkubwa kwa shirika hilo ili kuhakikisha malengo kusudiwa yanafikiwa na mwisho wake watu wengine wajifunze kutoka wilayani hapo.

Mapema Mwenyekiti mtendaji wa shirika hilo Samweli Mewama alisema shirika linalenga kuhakikisha jamii inaachana na mila potofu zianzochangia uvunjaji wa sheria ikiwemo ukeketaji.

“Tunalenga pia jamii kuelewa katiba ambayo ni sheria mama ,kuhimiza utawala bora na uwajibikaji  na kuyafundisha mabaraza ya ardhi ngaziza vijiji na kata”alisema.

Chanzo-Mwana wa Afrika blog.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa