Home » » MTUHUMIWA WA WIZI WA MIFUGO AUAWA KWA KUPIGWA MISHALE

MTUHUMIWA WA WIZI WA MIFUGO AUAWA KWA KUPIGWA MISHALE



Mwandishi wetu, Serengeti

MTU mmoja anayetuhumiwa kuwa mwizi wa  mifugo ambaye hajatambuliwa ameuawa na wakazi wa wa kijiji cha Nyamihuru kata ya Busawe wilayani Serengeti mkoani Mara baada ya kumteka mtoto aliyekuwa anachunga mifugo na kuondoka na kundi la mifugo.

Polisi wilaya hapa wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo novemba 17 majira ya kati ya saa 8 na 9 arasili mwaka huu katika katikati ya kijiji  cha Nyiboko na Marasomoche  na maiti kutelekezwa hapo ikiwa imejaa mishare ya sumu.

  Mifugo iliyokuwa imeibwa ni ng’ombe 43, mbuzi 14 na kondoo 12 mali ya Seba Marwa Magorombe mkazi wa Nyamihuru na amekabidhiwa mali yake.

Baadhi ya wakazi wa kijiji hicho waliiambia Redio Free Afrika kuwa baada ya kumteka mtoto anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 9 akichunga mifugo mmoja alifanikiwa kukimbia hadi nyumbani na kutoa taarifa.

Taarifa ya tukio ilisambazwa polisi na vijiji jilani wakati
wanafuatilia nyayo wakawakuta watuhumiwa wakiwa na mifugo na kuwashambulia na kufanikiwa kumuua mmoja na wengine wanasadikiwa kuwa wanne kufanikiwa kukimbia.

Polisi walikuta mwili wa marehemu  eneo la tukio huku ukiwa imesheheni mishare na kuuchukua hadi chumba cha kuhifadhia maiti hospitali teule ya Nyerere ddh ,kwa ajili ya taratibu zingine za kisheria ikiwa ni pamoja na utambuzi wa mtuhumiwa huyo.
 
Blogzamikoa
 

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa