Naibu waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu amesema,
serikali itahakikisha wote waliovamia hifadhi ya taifa ya tarangie wanachukulia
hatua za kisheria kwa haraka ili kuinusuru hifadhi hiyo.
Amesema uvamizi huo umechangia kwa kiwango kikubwa kukithiri kwa ujangiri kwa wanyama kama vile tembo na uhaibifu mwingine wa mazingira katika hifadhi hiyo.
Naibu waziri huyo wa maliasili na utalii, ametoa tamko hilo
kwenye kikao cha ujirani mwema kati ya kamati za ulinzi na usalama za
mikoa ya dodoma na manyara,zilizoketi, kutafuta ufumbuzi wa kutatua mgogoro
baina ya wavamizi katika pori la mkungunero lililoko mpaka wa hifadhi ya
taifa ya tarangire na mkoani manyara na dodoma.
Waziri nyalandu amesema,lengo la wizara yake ni kuona hifadhi za taifa zinalindwa kwa kiwango cha juu ili ziwe endelevu.
Mkuu wa Mkoa Wa Dodoma Dk Rehema Nchimbi na Mkuu Wa Mkoa Wa Manyara Elaston Mbwillo wamesma kuwa ili kuumaliza mgogo huo ni lazima mpaka wa eneo hilo lenye mgogoro uhakikiwe upya.
Pia wamesema ni lazima jamii iliyovamiwa eneo la hifadhi hiyo
ielimishwe ili kufahamu umuhimu wa hifadhi za taifa.
0 comments:
Post a Comment