Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Wakulima wameaswa kuondokana na kilimo cha mazoea, badala yake
watumie kanuni bora za kilimo ili waweze kuongeza kiwango cha
uzalishaji na kipato katika familia zao.
Mtafiti Mkuu wa Kituo cha Utafiti Seliani Arusha
(Sari), Steven Lyimo alisema hayo juzi kwenye maadhimisho ya Siku ya
Wakulima ya uboreshaji wa jamii ya mikunde kwa mazao mengi katika kilimo
mseto cha mahindi na mbaazi yaliyofanyika Kata ya Singe wilayani
Babati.
Alisema kutokana na mabadiliko ya tabianchi ya
eneo la Babati na Karatu, wakulima wanalazimika kutumia mbegu za muda
mfupi na kati ili waweze kupata wigo mpana wa uchaguzi wa mbegu
anapotaka kwenda shambani.
“Inatakiwa mwaka ambao hakuna mvua unapanda mbegu
ya muda mfupi, mwaka ambao kuna mvua kiasi unapanda mbegu ya muda wa
kati na mwaka ambao kuna mvua ya kutosha unapanda ya muda mrefu,”
alisema Lyimo
Chanzo:Mwananchi
0 comments:
Post a Comment