Home » » Mabadiliko ya tabianchi (Climate Change) yanavyoleta wimbi la magonjwa na wadudu kwenye zao la mahindi

Mabadiliko ya tabianchi (Climate Change) yanavyoleta wimbi la magonjwa na wadudu kwenye zao la mahindi

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

DSC_0459
Mkuu wa mradi wa utafiti Dk. Paul-Andre Calatayud, kutoka IRD/icipe, (kulia) akiwa tolea maelezo juu ya mdudu anayeharibu zao la mahindi, stem borer (Bungu/viwavi/funza) kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani) katika eneo la kijiji cha Kipuzi kwenye Kaunti ya Taita Taveta, Mombasa nchini Kenya.Kushoto kwake ni Joel ambaye ni mwenye shamba hilo lililo katika utafiti huo.
Na Andrew Chale, aliyekuwa Mombasa, Kenya
Imefahamika kuwa mimea mingi hasa mazao ya chakula inaandamwa na magonjwa ya aina mbalimbali yanayoleta usumbufu mkubwa na kurudisha nyuma kilimo pamoja na maendeleo kwa jumla hasa katika Bara la Afrika.
Changamoto hii unaweza kudhani inewakumba wakulima wa Tanzania pekee, la hasha hili ni tatizo linalowakabili wakulima katika nchi nyingi za kiafrika hasa zilizopo katika janga la Sahara.
Lakini swala la msingi la kujiuliza ni nini sababu ya kuongezeka kwa magonjwa hayo. “Kadri mvua inapokosekana tunaona magonjwa ya mazao nayo yanaongezeka na kuharibu mazao yetu” anasema Magret Mwasi mmoja wa wakulima kutoka kwenye kijiji cha Kipuzi kwenye Kaunti ya Taita Taveta, Mombasa nchini Kenya.
Mama huyu anakiri kuwa kuna uhusiano mkubwa kati ya kupungua kwa mavuno ya zao la mahindi na athari za mabadiliko ya tabianchi, lakini hakuna taarifa za kutosha kuwasaidia wakulima hao kukabiliana na changamoto hizo.
DSC_0374
Mmoja wa wakulima wa kijiji cha Kipuzi-Tait Hills, Bi. Magreth Mwasi akitoa maelezo kwa wandishi wa habari waliofika katika kijiji hicho kwa ajili ya kupata habari mbalimbali.
Hivi karibuni timu ya wandishi wa habari kutoka nchi mbalimbali za Afrika, ikiwemo Tanzania, Kenya, Rwanda, Madagascar, zaidi ya 10, wanaoandika katika mitandao ya kijamii (blogs), magazeti, radio walipata wasaha wa kufundishwa namna mabadiliko ya tabianchi yanavyoweza kuleta athari za mfumo wa Ki-ekolojia na Usalama wa Chakula Mashariki mwa Afrika.
Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na The French operator in media cooperation ( CFI) chini ya mradi wa Medias 21 2015, Africa & Asia, ikiwa ni juhudi za kutoa elimu ya mabadiliko ya tabianchi kuelekea mkutano wa kimataifa wa mazingira COP21, utakaofanyika nchini Ufaransa, wandishi waliweza kufundishwa kwa nadhalia na vitendo ambapo walipata wasaha wa kutembelea na kujionea maeneo hayo yaliyoatharika na magonjwa ya wadudu wanaoshambulia mazao ikiwemo mahindi.
DSC_0321
Pichani timu ya wandishi wa habari na wakufunzi ikipata maelezo ya awali wakati wa kujiandaa kuingia kwenye mashamba ya mahindi yaliyoathiriwa na wadudu aina Stem borer (funza), katika eneo la kijiji cha Kipusi-Taita Taveta, Mombasa Kenya.
DSC_0320
Mkuu wa mradi wa utafiti Dk. Paul-Andre Calatayud, kutoka IRD/icipe,akitoa maelezo juu ya mdudu anayeharibu zao la mahindi, stem borer (Bungu/viwavi/funza) kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani). kijiji cha Kipusi, Taita Hills-Taveta, Mombsa Kenya.
Taasisi ya ICIPE inafanya utafiti katika vilima vya Taita nchini Kenya chini ya mradi wa CHIESA ambao unalenga kujua mabadiliko ya tabianchi yanavyoleta athari katika kilimo hasa hasa zao la mahindi.
Mkuu wa mradi huo wa utafiti Paul-Andre Calatayud anasema magonjwa ya zao la mahindi yameongezeka kutokana na athari za mabadiliko ya tabianchi na kuathiri mfumo mzima wa kilimo na utekelezaji wake.
Anaeleza kuwa, mabadiliko ya tabianchi yanaweza kusababisha mtawanyiko na wingi wa wadudu waharibifu na hivyo kuharibu mazao ya nafaka mashambani na mavuno yake.
DSC_0419
Mkuu wa mradi wa utafiti Dk. Paul-Andre Calatayud, kutoka IRD/icipe,akiwa katika harakati za kuchunguza mahindi yaliyoharibiwa na mdudu aina ya Stem borer (viwavi/funza/bungua) katika moja ya mashamba eneo la Taita Hills, Mombasa nchini, Kenya.
DSC_0453
Mkuu wa mradi wa utafiti Dk. Paul-Andre Calatayud, kutoka IRD/icipe,akionyesha mdudu huyo anayeharibu zao hilo la mahindi akiwa amemshika mkononi akionyesha kwa wandishi wa habari (Hawapo pichani).
1882.400x400
Muhindi ulioharibiwa na mdudu aina ya Stem burer unavyoonekana pichani pamoja na picha chini..
A young maize tassel is opened up to reveal stem borers hidden inside, and damage caused by their feeding, in a farmer's field in Embu district, Kenya.   Stem borers are a class of insect pest, made up of a number of moth species distributed around the world, which lay their eggs at night on the underside of emerging leaves of young maize plants. The larvae, or caterpillars, that hatch from the eggs - i.e. the borers - quickly make their way inside the plant, where they feed undisturbed by predators. Young larvae feed on foliar tissue in the whorl, leading to perforations in unfolding leaves, and potential destruction of the growing point, while older larvae burrow into the stem, where they starve the growing plant of nutrients and can cause lodging. They feed extensively on tassels, ears, and stems. Borers' stealthy habits make them one of the most damaging pests for maize in Africa, and yet virtually invisible to farmers, who tend to attribute the damage to their crops to more visible pests. “Many farmers in Kenya don’t even know their maize fields have a stem borer problem, yet these insects cost them some 400,000 tons in lost harvest each year,” says CIMMYT maize breeder Stephen Mugo. Chemical pesticides can control borers, but must be applied soon after planting, and are difficult for resource-poor farmers to afford. “Even farmers who know about stem borers only notice the damage after it’s too late for chemical control. A seed-based technology is what we need,” says Mugo. In ongoing research, CIMMYT is collaborating with the Kenya Agricultural Research Institute (KARI) to develop maize varieties that are resistant to stem borers, and to disseminate these to resource-poor smallholder farmers. “Maize that resists stem borer damage would take the guesswork out of stem borer pesticide usage by eliminating it altogether,” says Mugo. The work is part of the Insect Resistant Maize for Africa (IRMA) project. For more information about stem borers in Kenya and CIMMY
DSC_0465
Wandishi wa habari wakipata wasaha wa kuuliza maswali kwa Dk. Paul baada ya kujionea jinsi wadudu hao aina ya Stem burer (funza) waliogundulika katika ukanda huo kuharibu mazao hayo ya Mahindi, eneo hilo la Taita Hills-Taveta, Mombasa Kenya.
“Utafiti wetu unalenga katika kupata suluhu ya kukabiliana na magonjwa ya mahindi, akiwemo funza (stem borer) ambaye amekuwa ni mharibifu sana katika zao la mahindi na baadae tutatoa majibu ya utafiti wetu ili uweze kutumiwa na wakulima hawa” anasema Paul
Wakulima mahindi katika vijini vinavyozunguka vilima vya Taita wameweka matumaini yao kwenye utafiti huo wakingoja kwa shauku kupata suluhu ya magonjwa na mahindi ambayo yamekuwa mwiba mchungu kwao.
DSC_0498
Mmoja wa wakulima kutoka kijiji cha Mbengoni, Nancy Makio akielezea namna ya wadudu hao wanavyoharibu mazao yao mashambani kwa wandishi wa habari waliofika katika kijiji hicho cha Mbengoni, Taita - MombasaKenya.
“Tuna matumaini makubwa na utafiti huu, tukiamini kwamba utakuja kutukomboa kutoka kwenye shida hii ya kukosa mazao kila mwaka” anasema Nancy Makio mmoja wa wakulima wa mahindi kutoka kijiji cha Mbengoni Kenya.
Magonjwa yanayoathiri mahindi ni mengi lakini mdudu funza ama bungua amekuwa ni tishio kubwa kwa mahindi sio tu Kenya bali hata hapa nyumbani Tanzania, hivyo kupatikana kwa njia ya kuangamiza mdudu huyo kutaleta tija kwa nchi zote za Afrika Mashariki
DSC_0445
wanahabari wakichanja mbuga katikati ya 'msitu' wa mahindi yaliyostawi kuelekea kwenye utafiti huo wa wadudu waharibifu wa zao hilo, eneo la Taita, Mombasa Kenya hivi karibuni...
DSC_0344
Shughuli za Kilimo zikiendelea..katika kijiji cha Kipuzi, Taita-Taveta, Mombasa Kenya.
DSC_0385
Zao la Mahindi likionekana kustawi katika eneo hilo la Taita-Taveta, Mombasa Kenya ambapo mahindi hayo yanakabiriwa na uharibifu mkubwa wa wadudu aina ya Stem borer kitaalam kama wanavyojulikana ambapo pia wakijulikana kama funza/viwavi ama bungua... ikitegemena na mahala husika kwa namna wanavyowahita
DSC_0356.jpgjjjj
Waandishi wa habari na bloggers wakizungumza na mmoja wa wakulima wa mahindi, Alfred Mwasi wa kijiji cha Kipusi akielezea juu ya wadudu hao wanavyoharibu zao hilo la Mahindi shambani mwake. Kulia ni Mwandishi Mwandamizi wa blog ya MODEWJIBLOG.COM, Andrew Chale (Tanzania), akifuatiwa na mwandishi wa habari na blogger, Sophie Dans (Kenya), mwandishi wa habari New Time Rwanda, Nkurunziza Michel (Rwanda) na Mwanablog ya Tabianchi, Dotto Kahindi (King Mandolin)-Tanzania ...
Aidham Taasisi hiyo ya icipe, iliweza kufanya utafiti wake huo katika vilima hivyo vya Taita, Mambasa nchini Kenya na utafiti mwingine ilifanya Mkoani Kilimanjaro, nchini Tanzania, ambapo pia waligundua wadudu hao waharibifu katika mazao huku wakisaidiwa na mashirika mbalimbali ikiwemo Chiesa upitia vyuo vishiriki kama Chuo kikuu cha Helsink (Finland), Chuo Kikuu cha York (Uingereza), Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM-Tanzania) na Chuo Kikuu cba Sokoine cha Kilimo (Tanzania).
projet_image_8
Ripoti hii ya imewezesha na CFI chini ya mradi wa Medias 21 Africa &Asia ( 2015), ikiwa ni juhudi za kutoa elimu ya mabadiliko ya tabianchi kuelekea mkutano wa kimataifa wa mazingira COP21.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa