Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti, ameanza rasmi kazi Mkoani humo kwa
kukagua ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro, ikiwa ni utekelezaji wa agizo la
Rais John Magufuli.
Mnyeti
alitembelea eneo hilo na mwenyeji wake mkuu wa wilaya hiyo mhandisi
Zephania Chaula na kamati ya ulinzi na usalama ya mkoa huo. Alipongeza
kasi ya maandalizi ya ujenzi huo kwani kila sehemu aliyokagua ambapo
ukuta utapita aliwakuta vijana hao wa JKT wana ari na hamasa ya utendaji
kazi.
"Kwa
namna vijana wetu wanajeshi wanavyoonekana kwenye maeneo yote
niliyopitia wanaonyesha wataimaliza kazi hii ndani ya muda mfupi tofauti
na agizo la miezi sita lililotolewa na Rais Magufuli," alisema Mnyeti.Aliwaahidi
kutoa ushirikiano kwa jambo lolote lile watakalokuwa wanalitaka kwenye
serikali ili kuhakikisha agizo hilo la Rais Magufuli linatekelezeka kwa
wakati husika.
Kamanda
wa operesheni ukuta Mirerani, Kanali Festus Mang'wela alimhakikishia
mkuu huyo wa mkoa kuwa vijana wote wanaojenga ukuta huo watafikishiwa
ujumbe huo wenye lengo la manufaa ya kulinda afya zao. Kanali
Mang'wela alisema ukuta huo wenye kilometa 24.5 na urefu wa mita tatu
kwenda juu unatarajiwa kuanza kujengwa rasmi Novemba 6 mwaka huu.
Alisema
wanatarajia mkuu wa JKT Meja jenerali Michael Isamuhyo ndiye atakuwa
mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo wa ukuta wanaotarajia kuujenga kwa muda
usiopungua miezi sita. Alitoa
shukrani kwa serikali ya wilaya ya Simanjiro kwa ushirikiano mkubwa
wanaowapa askari hao wakati wa utekelezaji wa zoezi hilo la maandalizi
ya ujenzi wa ukuta huo.
Katibu
Tawala wa wilaya ya Simanjiro, Zuwena Omary akisoma taarifa ya Wilaya
hiyo kwa mkuu wa mkoa huo alisema wanashirikiana ipasavyo katika
maandalizi ya ujenzi wa ukuta huo. Alisema
serikali ya wilaya ya Simanjiro na uongozi wa JWTZ wamekuwa na
mawasiliano ya mara kwa mara ili kuhakikisha zoezi hilo linafanyika
ipasavyo na kwa wakati muafaka.
Alisema
ukuta huo utachangia kudhibiti utoroshwaji wa madini hayo ambayo huuzwa
yakiwa ghafi au kusanifiwa na kuuzwa na madalali na wanunuzi wa ndani
na nje ya nchi. Alisema
katika utekelezaji wa agizo la Rais Magufuli, wamefanikisha uanzishwaji
wa ujenzi wa ukuta na kupatikana eneo la mnada wa madini ya Tanzanite
Mirerani.
"Hadi
hivi sasa imeshafanyika minada minne ya madini ya Tanzanite jijini
Arusha na serikali kuu na halmashauri ya wilaya ya Simanjiro zikapata
kodi ya mapato na kodi ya huduma ila minada ijayo itafanyika Mirerani,"
alisema Omary.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (wa pili kushoto) akitembelea kambi
ya wanajeshi wanaojenga ukuta wa kuzunguka madini ya Tanzanite Mji
mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro (kushoto) ni Mkuu wa wilaya hiyo
Zephania Chaula na (wapili kulia) ni msimamizi wa ujenzi huo kanali
Festus Mang'wela kwenye ziara yake ya kwanza Mkoani humo.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kushoto) akimsikiliza msimamizi wa
ujenzi wa ukuta unaojengwa kuzunguka madini ya Tanzanite Mji mdogo wa
Mirerani Wilayani Simanjiro, Kanali Festus Mang'wela, (katikati) baada
ya kutembelea zahanati ya kijiji cha Naisinyai ambapo madaktari wa JWTZ
wanatoa huduma za afya.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kulia) akikagua maandalizi ya
ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa
Mirerani Wilayani Simanjiro.
Mkuu
wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kushoto) akikagua maandalizi ya
ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa
Mirerani Wilayani Simanjiro.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti (kushoto) akikagua ramani ya ujenzi wa ukuta unaozunguka migodi ya madini ya Tanzanite Mji mdogo wa Mirerani Wilayani Simanjiro.
0 comments:
Post a Comment