Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Ofisa
elimu msingi wa Mji wa Babati Mkoani Manyara, Doroth Mwandila
akimkabidhi mwanafunzi wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira
English medium Vannesa Nada, cheti cha kuhitimu elimu ya msingi (kushoto) ni Mkurugenzi wa shule hiyo mhandisi Nada Narya.
Wanafunzi
wa darasa la saba wa shule ya msingi Deira English medium ya mjini
Babati Mkoani Manyara, wakionyesha mchezo wa kareti wakati wa mahafali
yao yaliyofanyika shuleni kwao.
Ili
kuondokana na tatizo la ukosefu wa ajili nchini, wanafunzi wametakiwa
kuyapenda masomo ya sayansi na hesabu ambayo yatawajengea uwezo wa
kupata ajira kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda.
Mkurugenzi
wa shule ya awali na msingi ya Deira English medium ya mjini Babati
Mkoani Manyara, mhandisi Nada Narya aliyasema hayo kwenye mahafali ya
pili ya darasa la saba na ya nane ya kumalizika elimu ya awali ya shule
hiyo. Mhandisi
Narya alisema shule hiyo imewaanda ipasavyo wanafunzi wa shule hiyo
kupenda masomo ya sayansi na hesabu ili kukabiliana na tatizo la ajira
kupitia kauli mbiu ya Tanzania ya viwanda hivyo wanafunzi wengine nchini
wapende masomo hayo.
Alisema
hivi sasa soko la ajira ni dogo na ili kuondokana na hali hiyo
inawapasa wanafunzi kuyapenda masomo sayansi na hesabu kwa lengo la
kujiandaa kwa nguvu zote katika kuhakikisha wanajipanga ipasavyo hivi
sasa ili baadae wachangamkia fursa ya ajili kupitia Tanzania ya
viwanda.
"Sisi
kama Deira tumeanza kuwaandaa wanafunzi wetu wapende masomo ya sayansi
na hesabu ili baadaye waweze kuendesha maisha yao kwenye soko la ajira
kwani wataalamu mbalimbali watatokea hapa shuleni kwetu," alisema
mhandisi Narya.
Mgeni
rasmi wa mahafali hayo, ofisa elimu ya msingi wa halmashauri ya mji wa
Babati, Doroth Mwandila alimpongeza mwanafunzi wa darasa la saba wa
shule hiyo, Edson Elias kwa kuongoza kwenye mtihani wa moku katika shule
37 za sekondari za halmashauri ya mji huo.
Mwandila
alisema ili kumuandaa kwa ajili ya masomo ya kidato cha kwanza mwakani,
anampa mwanafunzi huyo zawadi ya sh20,000 na atamnunulia vitabu,
madaftari na kalamu pindi akianza masomo yake kwa lengo la kumpa motisha
ya kusoma kwa bidii zaidi.
Aliwataka
wazazi na walezi wa wanafunzi wanaohitimu darasa la saba kwa mwaka huu,
kuwafuatilia watoto wao ipasavyo kwenye mienendo yao ya kila siku
wakiwa majumbani ili kuhakikisha wanawaanda vizuri kwa ajili ya kuanza
elimu ya sekondari mwakani.
Mwalimu
mkuu wa shule hiyo, Daniel Gaitu alisema shule hiyo ilianzishwa rasmi
Januari 2010 ikiwa na watoto watano, wavulana wawili na wasichana watatu
na hivi sasa ina wanafunzi 253 kati yao wavulana 119 na wasichana 134.
Gaitu
alisema kwa upande wa taaluma, shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri kwenye
mitihani kwani wanafunzi wa darasa la nne walifanikiwa kushika nafasi
ya kwanza kwenye halmashauri ya mji huo katika mtihani wa Taifa wa mwaka
2013, 2014 na nafasi ya pili mwaka 2016.
Alisema
wanafunzi wa darasa la saba wa mwaka jana walishika nafasi ya kwanza
kwa mtihani wa Taifa kwenye halmashauri ya mji huo na darasa la saba wa
mwaka huu wameshika nafasi ya kwanza kwenye mtihani wa moku mkoa wa
Manyara kwenye shule 37 za halmashauri ya mji wa Babati.
0 comments:
Post a Comment