Mkoa wa Manyara una eneo la hekta 1,568,117 zinazofaa kwa
kilimo ambapo zaidi ya hekta 867,500 zinatumika kwa kilimo cha mazao ya
aina mbalimbali. Eneo la kilimo linabadilika kila msimu kulingana na
malengo ya wakulima na mwelekeo wa hali ya hewa.
Pia Mkoa una maeneo yanayofaa kwa kilimo cha umwagiliaji yanayofikia
hekta 30,997 na kati ya hizo hekta 11,715 zinatumika kuzalisha mazao ya
aina mbalimbali kama vile mahindi, mpunga, miwa, migomba na mazao ya
mbogamboga na matunda. Maeneo makubwa yapo Wilaya ya Babati (Bonde la
Kiru) na Simanjiro (Ukanda wa Mto Pangani). Maeneo mengine yapo Mbulu
(Bonde la Bashay) na Hanang (Bonde la Endagaw na Gocho)
Mazao yanayolimwa ni Mahindi, Alizeti, Mbaazi, Mtama, Ngano,
Maharage, Miwa, Vitunguu Maji, Vitunguu Saumu na Mpunga ambayo hutumika
kama mazao ya Biashara na Chakula kwa wakazi wa Mkoa. Ziada ya
uzalishaji huuzwa kwenye Mikoa mingine na Nchi jirani za Kenya, Somalia,
Ethiopia, Eritrea na Sudani.
Moja ya Mashamba ya Mahindi Wilayani Hanang-Mkoa wa Manyara
Moja ya Mashamba ya Mbaazi Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara
Moja ya Mashamba ya alizeti katika Wilaya ya Kiteto Mkoa wa Manyara
Shamba la Ngano katika Wilaya ya Hanang-Mkoa wa Manyara
Mafanikio yaliyopatikana katika Sekta hii yanatokana na jitihada za
Serikali na wadau wa maendeleo katika kuimarisha matumizi ya wanyama
kazi, matrekta makubwa na madogo (power Tillers), mbegu bora, mbolea na
wataalam wa ugani.
Maksai wakitumika kusafirisha mazao shambani
Mwaka 2006, Serikali ilianzisha Mpango wa kilimo wa ASDP kwa lengo la
kuongeza uzalishaji mazao kwa kushirikiana na Mradi wa PADEP
“Participatory Agriculture Development and Empowerment Project”
unaoshirikisha wananchi kuibua Miradi ya Vikundi na Miradi ya Jamii na
kuchangia gharama za utekelezaji katika Sekta za Kilimo na Mifugo.
Miundombinu mbalimbali iliweza kujengwa katika maeneo mengi ya Mkoa.
Baadhi ya miundombinu hiyo ni Vituo vya rasilimali za Kilimo na Mifugo, Maghala, majosho, nyumba za maafisa ugani na machinjio.
Aidha, Mkoa unashirikiana na Mashirika na Taasisi za Maendeleo ya
kilimo katika kukuza na kuendeleza Sekta ya Kilimo na Mifungo. Mashirika
hayo yametajwa katika jedwali lifuatalo na kuonesha majukumu
wanayotekeleza.
Chanzo Tovuti ya Mkoa wa Manyara
Chanzo Tovuti ya Mkoa wa Manyara
0 comments:
Post a Comment