Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (kulia) akimkabidhi nahodha wa timu ya Qatajiring zawadi mbalimbali mara baada ya kuibuka kidedea baada ya kuifunga timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.
Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay akiongea na Wananchi wakati wa kuhitimisha fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu.
Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Anastazia Wambura (aliyevaa miwani) akikagua timu za Qatajiring na timu ya Zahanati wakati wa fainali za Flatei Jimbo Cup wilayani Mbulu. Katikati ni mdhamini wa mashindano hayo Mbunge wa Mbulu Vijijini Flatei Massay.
Na Eleuteri Mangi, WHUSM, Mbulu
Halmashauri
zote nchini zimetakiwa kutenga maeneo ya michezo wakati wa kupanga
mipango miji kwa matumizi bora ya ardhi katika maeneo yao.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na
Michezo Anastazia Wambura alipokuwa akifunga fainali ya mashindano ya
Jimbo Cup inayodhaminiwa na Mbunge wa Jimbo la Mbulu Vijijini Mhe.
Mbunge wa Mbulu Vijijini, Flatei Massay iliyochezwa katika eneo la kata
ya Dongobesh Wilaya ya Mbulu Mkoani wa Manyara.
“Natoa
wito kwa Halmashauri zote ikiwemo halmashauri yenu ya wilaya ya Mbulu
wakati wa kupanga matumizi bora ya ardhi kwa ajili ya mipango miji
mkumbuke kutenga maeneo ya michezo, Baraza la Michezo la Taifa litatoa
mafunzo ya michezo na utaalam” alisema Naibu Waziri Wambura.
Akikabidhi
zawadi za washindi katika mashindano hayo ambao ni timu ya Qatajiring
kutoka kijiji cha tumati ambao ni mshindi wa kwanza na timu ya Zahanati
kutoka kijiji cha Diomati mshindi wa pili, Naibu Waziri Wambura
amewahimiza wachezaji na wananchi kuthamini michezo kwa kuwa ni ajira,
inaleta umoja na mshikamano miongoni mwa jamii.
Dakika
90 za fainali hizo ziliisha kwa timu zote kufungana bao 2-2 na hatimaye
timu ya Qatajiring iliibuka kidedea kwa ifunga timu ya Zahanati kwa
penati 4-1.Akionesha umuhimu na umahiri wa wilaya ya Mbulu katika
michezo, Naibu Waziri Wambura amesema wilaya hiyo imekuwa kitovu cha
wanamichezo bora hasa mchezo wa riadha ambao wameiletea sifa Tanzania
ndani na nje ya nchi.
0 comments:
Post a Comment