Naibu Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisalimiana na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky) mara baada ya kuzuru katika kiwanda hicho kilichopo katika eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara. (Picha Zote Na Mathias Canal)
Naibu
Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa (Katikati) akisikiliza kwa makini
taarifa kuhusu utekelezwaji wa maagizo ya waziri Mkuu mara baada ya
kutembeleaa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and
Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky).
Naibu
Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akisikiliza kwa makini taarifa
kuhusu utekelezwaji wa maagizo ya waziri Mkuu mara baada ya kutembeleaa
kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg
Pardeep Singh Hans (Tosky).
Muonekano wa vitendea kazi vya kiwanda cha Mbolea cha Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd).
Naibu
Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea
Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep
Singh Hans (Tosky).
Naibu
Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea
Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep
Singh Hans (Tosky).
Naibu
Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea
Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep
Singh Hans (Tosky).
Naibu
Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa akikagua kiwanda cha Mbolea
Minjingu akiongozwa na Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda hicho Ndg Pardeep
Singh Hans (Tosky).
Muonekano wa baadhi ya vitendea kazi vya Kiwanda cha mbolea cha Minjingu kilichopo eneo na Kata ya Minjingu Mkoani Manyara.
Na Mathias canal, Manyara
Naibu
Waziri wa kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ametembelea kiwanda cha mbolea cha
Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) kilichopo katika eneo na
Kata ya Minjingu Mkoani Manyara ambapo pamoja na mambo mengine amejionea
hali ya uzalishaji wa mbolea asilia ya kupandia aina ya Minjingu.
Mhe
Mwanjelwa alitembelea kiwandani hapo ambapo miongoni mwa matakwa yake
ilikuwa ni pamoja na kufatilia maagizo ya Waziri Mkuu wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania, Mhe Kassim Majaliwa aliyoyatoa mwishoni mwa mwezi
Februari mwaka huu alitembelea eneo la machimbo ya mbolea ya Minjingu na
kupokea taarifa ya uendeshaji wa Kiwanda cha Mbolea cha Minjingu.
Mhe
Mwanjelwa alishuhudia uzalishaji ukiwa umeongezeka kufikia Tani 150,000
kwa mwaka ambapo uongozi wa kiwanda hicho umetii agizo la Waziri Mkuu
la kuwasihi kuboresha teknolojia ili kuzalisha Tani zaidi ya 150,000
ambazo zitaongeza kiwango cha upatikanaji wa mbolea hapa nchini kwwani
bado upo chini kuliko mahitaji
Katika
hatua nyingine Uongozi wa kiwanda hicho ulitii agizo la Mheshimiwa
Waziri Mkuu ambaye aliwagiza kuandika barua kwa Mhe Rais wa jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Dkt John Pomnbe Magufuli kuomba radhi kwani mifuko
waliyokuwa wanatumia kuuzia Mbolea hiyo ya Minjingu ilikuwa na nembo ya
nchi ya Kenya licha ya kuwa inazalishwa hapa nchini.
Hata
hivyo Mhe Mwanjelwa alijionea mifuko hiyo ikiwa imebadilishwa na kuwa
na muonekano wa anuani ya Tanzania kama uzalishwaji wake ulivyo.
Sambamba
na hayo pia Naibu Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa ameutaka uongozi
wa kiwanda hicho cha mbolea Minjingu (Minjingu Mines and Fertilizer Ltd)
kutoa elimu kwa umma juu ya ubora na umuhimu wa mbolea hiyo ya
kupandia.
Mbolea
hiyo inatokana na miamba inayochimbwa katika eneo la Minjingu Mkoani
Manyara ambayo husagwa na kufungashwa kwenye kiwanda kilichojengwa
katika eneo hilo. Mbolea ya Minjingu imeboreshwa kwa kuongezwa
virutubisho vya Nitrogen, Salfa, Magnesi, Zinki na Boron (N, S, Mg, Zn,
na B).
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kiwanda cha Mbolea cha Minjingu
(Minjingu Mines and Fertilizer Ltd) Ndg Pardeep Singh Hans (Tosky)
ameiomba serikali kupitia wizara ya kilimo kuwaruhusu maafisa ugani kote
nchini kupatiwa mafunzo maalumu yatakayowaimarisha ili waweze kuwa
sehemu ya kuitangaza mbolea bora ya Minjingu ambayo inazalishwa nchini.
Alisema
kuwa serikali inapaswa kutazama upya utozaji wa VAT kwa wazalishaji wa
bidhaa mbalimbali hapa nchini kwani tozo ya VAT ya asilimia 18
wanayotozwa ni kubwa huku waagizaji wa mbolea nje ya nchi wao wanaingiza
pasipo tozo kama hiyo.
Aidha,
alisema kuwa tayari makala za vipindi vya Redio, Televisheni na
Magazeti mbalimbali zimeanza kuandaliwa kwa ajili ya kuelimisha wakulima
juu ya umuhimu wa mbolea hiyo ya Minjingu ambayo ni bora kuliko mbolea
nyingine yoyote nchini na nje ya nchi.
Naibu
Waziri wa Kilimo Mhe Mary Mwanjelwa alisema kuwa serikali ya awamu ya
tano inayoongozwa na Mhe Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt
John Pombe Magufuli imejidhatiti katika viwanda hivyo inathamini bidhaa
zinazozalishwa na viwanda vya ndani.
0 comments:
Post a Comment