Ikiwa
unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu
blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema mgombea urais wa Chama cha Demokrasia na
Maendeleo (UKAWA), Bw. Edward Lowassa na vyama vinavyounda Umoja wa Katiba ya
Wananchi (UKAWA), wajiandae kushindwa katika Uchaguzi Mkuu, Oktoba 25,
mwaka huu.
Kimesema
wapambe wa Bw. Lowassa walimdanganya na kumshawishi ahame CCM kwenda CHADEMA
akidai waliomshawishi walimpoteza.
Kauli hiyo
imetolewa Dar es Salaam jana na Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM Taifa,
Bw. Nape Nnauye wakati akizungumza na waandishi wa habari juu ya ushiriki wao
katika uchaguzi huo na nafasi ya ushindi.
Alisema
CCM kinaamini kuwa, baada ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kumtangaza
mshindi wa nafasi ya urais, viongozi wa UKAWA wajiandae kupelekwa majumbani
mwao kwa gari la kubebea wagonjwa.
Aliongeza
kuwa, CCM haishindani na wapinzani bali inashindana na makapi akisisitiza kuwa,
hao wanaojiita wapinzani wametokea CCM; hivyo Tanzania hakuna mpinzani.
"Yanga
ikicheza na Lipuli, kila mtu anajua matokeo yatakuwaje hivi sisitunajua matokeo
yetu wazi...tuna nafasi kubwa ya ushindi kwa asilimia zote na tutashinda
asubuhi kweupe kabla ya Oktoba 26, mwaka huu," alisema.
Bw. Nnauye
alisema; "Augustino Mrema wakati anahama CCM kwenda NCCR-Mageuzi mwaka
1995, aliondoka kwa mwembwe kama hizi ambazo tunaziona, lakini kilichotokea,
nadhani kila mtu alikiona," alisema.
Alifafanua
kuwa, chama hicho hakifanyi kazi kwa shinikizo la mtu; bali kinazingatia sheria
na kanuni za chama zinavyosema akidai anayetaka kuondoka CCM, aondoke ila chama
kitaendelea kuwepo.
Akizungumzia
majimbo yaliyowekwa kiporo na Halmashauri Kuu yachama hicho, alisema baada ya
vikao vyao kumalizika Mjini Dodoma,kazi iliyobaki ni kuyajadili majimbo 11
yaliyokuwa yamebaki.
"Hadi
sasa, Kamati Kuu imeyajadili majimbo tisa na bado inaendelea na vikao ili
kuyamaliza yote...majimbo yanayoendelea kujadiliwa ni Singida Mashariki na
Kiteto, mkoani Manyara," alisema.
Aliwataja
walioshinda katika majimbo tisa kuwa ni Jerry Silaa (Ukonga),Edward Mwalongo
(Njombe Kusini), Venance Mwamoto (Kilolo), Raphael Chegeni (Busega), Edwin
Ngonyani (Namtumbo), Mohamed Mchengerwa(Rufiji), Norman Sigalla (Makete),
Martin Msuha (Mbinga Vijijini) na Joel Mwaka (Chilonwa).
CHANZO MAJIRA
0 comments:
Post a Comment