DAKTARI wa Hospitali ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara, Dk Godson
Kato amehukumiwa kifungo cha mwaka mmoja jela au kulipa faini ya Sh
200,000 baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la matumizi mabaya ya nyaraka
na kujipatia Sh 800,000 za mwajiri wake.
Dk Kato alisomewa hukumu hiyo juzi ya kwenye mashtaka ya matumizi
mabaya ya fedha za umma na Hakimu wa Mahakama ya wilaya hiyo Majid Hudi,
ambapo alilipa faini hiyo Sh 200,000 na kuachiwa huru.
Hata hivyo, mshtakiwa wa pili wa kesi hiyo namba 409/2012, Charles
Simon ambaye ni Mhasibu Msaidizi wa Halmashauri ya wilaya hiyo
aliyeidhinisha Dk Kato kupatiwa fedha hizo, aliachiwa huru baada ya
kuonekana hana hatia.
Awali, mwendesha mashtaka wa kesi hiyo Isidore Kyando wa Taasisi ya
Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (Takukuru) mkoani Manyara, alisema
kuwa Dk Kato alitenda kosa hilo Novemba 20 mwaka 2012.
Kyando alisema Dk Kato aliomba kwa mwajiri wake ambaye ni Halmashauri
ya wilaya ya Kiteto fedha hizo Sh 800,000 kwa ajili ya kwenda katika
semina hewa vijijini na mhasibu huyo Simon akashirikiana na mhalifu
kumwidhinishia fedha hizo.
Alisema mganga huyo aliandaa semina hewa huko vijijini na kuomba
kiasi hicho cha fedha Sh 800,000 kwa jili ya kutoa elimu kwa wananchi na
akapatiwa fedha hizo, ila hakutimiza hilo aliloliombea ambapo
alijinufaisha yeye mwenyewe.
Akitoa hukumu hiyo Hakimu Hudi alimhukumu Dk Kato kwenda jela kwa
kutumikia kifungo cha mwaka mmoja au kulipa faini ya Sh 200,000 kwa kosa
hilo ambapo alizilipa na mshtakiwa wa pili Mhasibu Simon aliachiwa
huru.
0 comments:
Post a Comment