Home » » ULINZI SHIRIKISHI WAPUNGUZA UHALIFU MANYARA

ULINZI SHIRIKISHI WAPUNGUZA UHALIFU MANYARA

Na Fortunatha Ringo, Manyara
KAMANDA wa Polisi Mkoa wa Manyara, Liberatus Sabas amesema mpango wa ulinzi shirikishi umechangia kwa kiasi kikubwa kupunguza hali ya uhalifu mkoani Manyara kwa zaidi ya asilimia 85.

Akizungumza na waandishi wa habari mkoani humo jana Kamanda Sabasi alisema wananchi mkoani humo wamekuwa na ushirikiano na Jeshi la Polisi katika kufichua mambo ya uhalifu tofauti na awali.

Alisema kuwa uhalifu uliopungua zaidi ni unywaji, na utengenezaji wa pombe haramu ya moshi aina ya gongo.

Alisema wananchi wenyewe wamekuwa na utaratibu wa kuwakamata wahalifu na kuwafikisha katika vyombo vya dola.

“Kipindi cha Januari hadi Desemba, mwaka jana kuliripotiwa makosa mbalimbali katika wilaya zote mkoani Manyara ambapo Jumla ya makosa yaliyoripotiwa ni 2,143 idadi hii ya makosa inajumuisha makosa dhidi ya binadamu, makosa ya kuwa ni mali na makosa dhidi ya maadili ya jamii.

“Idadi hii ya makosa ya mwaka 2011 ukilinganisha na Makosa -2278 ya mwaka 2010 inaonyesha makosa yamepungua,” alisema.

Alisema kuwa uchunguzi umebaini kuwa matukio mengi yanakwenda sanjari na unywaji wa pombe haramu ya moshi aina ya gongo na baadhi ya makosa hutokana na mila na desturi za kutembea na silaha za jadi katika mikusanyiko ya watu.
Chanzo: Mtanzania

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa