Na Mohamed Hamad, Manyara Yetu
Watu watatu wamefariki dunia na wengine watano kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto mkoani Manyara baada ya kuvamiwa na kundi la watu wanaodaiwa kuwa ni wafugaji (wamasai) usiku kuamkia Augst 10 mwaka huu
Kwa mujibu wa Bw.Yahaya Masumbuko Diwani wa kata ya Bwagamoyo aliyekuwa katika eneo hilo alisema tukio hilo limetokea Augost 9 saa nane usiku wakati wakulima hao wakiwa wamelala katika eneo la pori kwa pori namba moja
Bw. Masumbuko alisema matukio hayo yamekuwa yakijitokeza mara kwa mara kutokana na pande hizo kugombea ardhi huku viongozi wakionekana kutokuwa na dhamira za dhati kutatua mgogoro huo
Mtoto mmoa aliyetambuliwa kwa jina la Daudi Mzanaki (14) amefariki Dunia huku wengine waliojeruhiwa kuwa ni Msafiri Songoro, aliyechomwa mshale wa mgongoni na puani,Msumari Gulile aliyepigwa rissai mgongoni
Wengine ni Lazaro Paulo aliyepigwa risasi kiunoni na Manesa Charles aliyepigwa risasi pajani na kukatwa na sime jichoni ambao kwa pamoja wamelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto kwa matibabu zaidi
Hata hivyo baadhi ya wafugaji walilimbia gazeti hili kuwa awali walichangishwa fedha kwaajili ya kuwaondoa wakulima katika maeneo hayo lakini hawakuweza kuondoka kwa muda mrefu hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwao
“Tumekuwa tukikosa maeneo ya kuchungia mifugo yetu hata viongozi wanajua lakini limenyamaziwa kwa muda mrefu huku tukigombana mara kwa mara na wakulima kwa kugombea ardhi”alisema mmoja wa wafugaji hao ambaye hakutaka kujatwa jina
“Wafugaji tulichangishwa fedha nyingi sana kwaajili ya kuwaondoa wakulima lakini cha kushangaa aliyetuhamasisha alikuwa mkuu Wilaya Frank Uhahula ambaye hakubahatika kuteuliwa na Rais baada ya badiliko la Ma DC”kilisema chanzo kimoja cha habari hizi
Katika tukio hilo Diwani Masumbuko alisema wafugaji hao walivamia kitongozji cha pori kwa pori usiku wa saa nane wakiwa na silaha za moto ambapo walianza kupiga juu hatimaye kuchoma moto nyumba za wakulima hao
Alisema wakati wahanga wa tukio hilo wakikimbia wengine walichomwa mikuki,kupigwa risasi na kuchomwa mishale na hata baada ya kudondoka waliendelea kupigwa kwa fimbo katika sehemu mbalimbali za miili yao
Awali alizungumza na majira Bw. Kiyondo Seboa (Suruti) alisema augosti 9 mwaka huu mmoja wa wakulima alifika kwake kuomba msaada wa kwenda kuokamata mifugo ng’mbe zaidi 1500 zikiwa shambani zikila mazao
Alisema baada ya kukamatwa mifugo hiyo wafugaji hao hawakujitokeza ndipo wakatoa taarifa polisi hatimaye kufika ambapo hata hivyo waliondoka na kuagiza kuwa wahalifu wakifika wakamatwe na kufikishwa kituoni
Hata hivyo ilipofika usiku wa saa nane walifika wafugaji hao wakiwa na silaha kali na kupiga juu huku wakichoma moyo makazi wa wakulima hao ambapo zaidi ya nyumba saba zailichomwa moto huku zingine zikiwa na vyakula ,pikipiki ,baiskeli, na bidhaa zingine
Hata hivyo kwa mujibu wa Ofisa mtendaji wa kijiji cha Kimana Bw.Bakari Lugage akiwa na Askari hao alisikika akisema wakulima hao ni wavamizi katika maeneo hayo hivyo hawakupaswa kuwepo hapo
Kwa upande wake Diwani Masumbuko alisema, anashangazwa na viongozi wa Serikali kutoa matamko ya jumla pale yanapojitokeza matatizo lakini kabla ya tatizo siku zote huwa kimya kana kwamba hakuna tatizo ndani ya Kijiji
Kwa mujibu wa taarifa toka katika Hospitali ya Wilaya ya Kiteto hali ya majeruhi bado sio shwari wakisema kuwa wengi wao wamekatwa katwa kwa sime pamoja na kupigwa kwa fimbo wakati wakijaribu kukimbia
Mauaji ya mara kwa mara wilayani kiteto yameendelea kujitokea kutokana na wakulima na wafugaji kugombea ardhi ambayo pande hizo mbili huitumia kwa njia ya kujipatia kipato wakati wakulima wakiitumia kwa kulima na wafugaji kuchungisha mifugo yao
Blogzamikoa
0 comments:
Post a Comment