na Efracia Massawe, Simanjiro
WANAKIJIJI
wa eneo la Naisinyai wilayani Simanjiro mkoani Manyara wameondokana na adha ya
tatizo la maji lililokuwa likiwakabili kwa muda mrefu, baada ya Kampuni ya
TanzaniteOne kujenga kisima cha kusafisha maji katika eneo hilo.
Akizungumza
na Tanzania Daima kutoka Manyara jana Ofisa uhusiano wa Kampuni hiyo, Dotto
Medard alisema kuwa kampuni hiyo imechukua jukumu la kujenga na kukabidhi
kisima hicho kwa kituo cha Polisi ‘post’ kwa ajili ya matumizi ya kijiji.
Aidha,
alitanabanaisha kuwa kisima hicho kimegharimu sh milioni 60 na kitakuwa msaada
katika wilaya hiyo hususan katika kusafisha maji yanayotoka katika mabomba
mbalimbali kwani kijiografia eneo hilo lina maji chumvi ambayo nayo si salama
kwa matumizi.
“Kushirikiana
na kijiji si mara yetu ya kwanza, hata hivyo mara nyingi tunashirikiana na
viongozi husika kabla hatujafanya jambo lolote, hivyo kisima hiki kitatumiwa na
wanakijiji wa ndani na nje ya eneo hili,” alifafanua Medard.
Naye
Mkuu wa mkoa huo, Erasto Mbwilo, alitabanaisha kuwa msaada wa kampuni hiyo
umekuja wakati muafaka kwa sababu mbali na wanakijiji hao kutumia maji chumvi,
lakini bado serikali haikubaliani ni lini ingetatua tatizo hilo.
Chanzo: Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment