Home » » KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA PEMBEJEO

KIZIMBANI KWA TUHUMA ZA WIZI WA PEMBEJEO

AFISA  kilimo na Mifugo wilaya ya Serengeti ,wazabuni wa pembejeo ,watendaji wa vijiji,na wakulima wamefikishwa katika Mahakama ya wilayaya Serengeti mkoani Mara,wakikabiliwa na makosa 50 ya wizi wa fedha za
Pembejeo zenye thamani ya tsh,315,840,000=

Mbele ya  hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama hiyo Amon Kahimba
,mwendesha mashitaka  Mkaguzi Msaidizi wa Polisi Abdallah Idd
amewataja Washitakiwa kuwa ni  Andrew Manyerere (55) Afisa
kilimo/Mifugo wilaya, Nyitamboka Kitang’ita (61)wa kijiji cha
Majimoto, Karebu Ruji(41), Paulo Nyandito (50) wote wafanyabiashara wa
pembejeo.

Wengine ni Joseph Petro (38) Afisa Mtendaji kijiji cha Rwamchanga,
Damiani Nyamaheda (34) hakuwepo Mahakamani baada ya kutoroka, Emmanuel Mkamba (29)  mkulima mkazi wa kijiji cha Itununu na Pili Nyakimori
(35) mkulima.

Mwendesha mashitaka ameiambia Mahakama  kuwa mwaka 2012 kwa nyakati tofauti katika vijiji vyao wanavyofanyia kazi mshitakiwa wa pili hadi
wa nane wanatuhumiwa kula njama, kugushi sahihi za watu na kuchukua
fedha za pembejo na kufanya tendo la wizi.

Kwa mshitakiwa  wa kwanza katika shauri hilo Andrew Manyerere ambaye
ni Afisa kilimo na mifugo wilaya ya Serengeti anashitakiwa kwa kosa la
uzembe baada ya kushindwa kuchukua hatua za kudhibiti wizi huo mapema.
Washitakiwa  wamekana  mashitaka yanayowakabili ,na wako nje kwa
dhamana  baada ya kutimiza masharti ya kila mmoja kuwa na wadhamini
wawili wanaoaminika hadi  aprili 23 mwaka huu kesi hiyo  itakapotajwa
tena.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa