Babati. Mfuko wa Pensheni wa Serikali za Mitaa, LAPF, umekabidhi misaada mbalimbali kwa Hospitali ya Hydom, mkoani Manyara.
Misaada hiyo ya vyandarua, mashuka 300 na
mablanketi 150 vyote vikiwa na thamani ya Sh5 milioni vilikabidhiwa na
Meneja wa LAPF Kanda ya Kaskazini, Rajab Kinande juzi.
Kinande alisema LAPF imekabidhi msaada huo kwa ajili ya wodi ya watoto ikiwa ni sehemu ya mrejesho wake kwa jamii inayoizunguka.
Alisema ana imani watoto watapata huduma nzuri na
kuimarisha afya zao kwa maendeleo yao... pia tunasaidia sekta ya
michezo, kulea yatima na elimu,” alisema.
Mkurugenzi wa hospitali hiyo, Dk Olav Espegren
alisema msaada wa LAPF umekuja kwa wakati mwafaka na kwamba, utasaidia
kwa kiwango kikubwa kuboresha huduma hospitalini hapo.
“Ni mwaka mmoja tangu Hydom kuwa wadau wa LAPF na imeonyesha jinsi inavyowajali wadau wake,” alisema.
Dk Espegren alisema hivi sasa tatizo kubwa linalokabili hospitali hiyo ni upungufu wa waganga na wauguzi.
Hospitali hiyo imekuwa kimbilio kwa Wilaya za
Manyara na mikoa mingine ambazo zipo karibu, kutokana na huduma
zinazotolewa. Watumishi wa hospitali hiyo ni wachangiaji wa mfuko huo
ambao unaongoza kwa kuweka vizuri hesabu zake.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment