Babati. Wakulima wa ufuta kwenye kata tano za Tarafa ya Mbugwe, wilayani Babati, mkoani Manyara, wanatarajia kunufaika na kilimo hicho msimu huu baada ya kulima na kupanda mbegu kwenye ekari 5,625 za mashamba yao.
Ofisa Mazao wa Shirika la Farm Africa, Tumaini Elibariki alisema wakulima hao wanatarajia kupata mavuno ya tani 2,390 za ufuta.
Elibariki alisema wakulima kumi wa ufuta kata za
Mwada, Magugu, Magara, Nkaiti na Kiru, awali walilima na kupanda kilo
11, 250 sawa na tani mbili za ufuta.
Chanzo:Mwannchi
Chanzo:Mwannchi
0 comments:
Post a Comment