Home » » RC ATAKA WATUMISHI KUWA WAADILIFU NA KUFUATA SHERIA

RC ATAKA WATUMISHI KUWA WAADILIFU NA KUFUATA SHERIA

Manyara.Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Eraston Mbwilo, amewataka wafanyakazi mkoani humo kufanya kazi kwa uadilifu na kufuata sheria kwa kutoa huduma stahiki kwa wateja wao, ili kuboresha ufanisi wa kazi zao.
Wito huo ameutoa jana wakati wa baraza la kwanza la wafanyakazi la mwaka 2014 la mkoa huo, ambapo alisema wafanyakazi huongozwa na sheria hivyo hawana budi kuzifuata.
Awali akifungua baraza hilo, Mbwilo alisema, wafanyakazi wengi hawazingatii sheria na uwajibikaji katika kazi zao hususani suala la muda, kwani wapo watu waliojenga mazoea ya kuchelewa kuingia na kuwahi kutoka kazini.
“Wafanyakazi tunahitajika kuzingatia muda wa kuingia ofisini kwa kuwa sheria zinatubana lakini tunawaonea sana wahudumu wa ofisi, hawa ndiyo sheria zinawabana zaidi maana wanawahi kuingia kazini, utakuta saa 1.30 muhudumu tayari anafanya usafi,” alisema Mbwilo. Alilitaka baraza hilo kujadili suala la uadilifu kwa wafanyakazi ikiwa ni pamoja na matumizi ya lugha nzuri na zenye kuridhisha za kuwaweka karibu zaidi na wateja pindi wanapofuata huduma kwenye ofisi zao.
Chanzo:Mwananchi

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa