Mkoa wa Manyara kwa mwaka umekadiria kutumia Sh165.3 bilioni kwa
ajili ya kutengeneza bajeti yake ya miaka ya 2014/15 na 2016/17.
Katibu Tawala Msaidizi (Mipango na Uratibu) Samwel Tenga, alisema Sh128.23 bilioni katika fedha hizo, ni za matumizi ya kawaida.
Tenga alisema kiasi kinginge cha Sh37.07, bilioni ni kwa ajili ya kugharimia utekelezaji wa miradi ya maendeleo.
Katibu huyo alisema Sh10.58 bilioni katika fedha
za matumizi ya kawaida, zitatokana na vyanzo vya mapato vya ndani vya
mamlaka za serikali za mitaa.
Alisema ingawa bajeti inayoidhinishwa inashuka
kila mwaka, lakini kuna changamoto kadhaa zilizojitokeza katika
uidhinishaji wa bajeti hiyo.
Alisema katika kipindi cha miaka mitatu (3)
iliyopita ofisi ya mkuu wa mkoa iliidhinisha Sh8.228 za maendeleo lakini
zilitolewa Sh5.058, bilioni kwa ajili ya matumizi ya kawaida.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment