Home »
» Mazao mbalimbali kuvunwa karibuni
Mazao mbalimbali kuvunwa karibuni
JUMLA
ya tani 450,330 za mazao ya chakula na tani 51,930 za mazao ya biashara
ya wakulima zinatarajiwa kuvunwa wilayani Simanjiro, mkoani Manyara,
baada ya kulima hekta 148,935 za mazao ya biashara na hekta 51,930 za
mazao ya chakula.
Akisoma taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Manyara,
Elaston Mbwilo, Katibu Tawala wa wilaya hiyo, Elias Ntiruhungwa,
aliyasema hayo jana wakati akisoma taarifa ya wilaya ya Simanjiro kwa
mkuu wa mkoa huo Elaston Mbwilo, kwenye ziara yake ya kukagua miradi
mbalimbali ya maendeleo.
Ntiruhungwa alisema hadi mwishoni mwa
Desemba mwaka jana wilaya hiyo ilikuwa imepata wastani wa mvua milimita
58 ambayo ni kidogo kwa shughuli za kuandaa mashamba na kusababisha
wakulima wengi kushindwa kuyatayarisha.
Hata hivyo, alisema wilaya
hiyo imekwisha sambaza vocha za pembejeo za ruzuku kwa wakulima wa
vijijini katika utekelezaji wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) wilayani humo.
Kwa upande wake, mkuu wa mk o a h u o , Mbwi l o aliwataka viongozi
wa wilaya hiyo kuwahesabu wafugaji ili kuondoa dhana ya wakazi wa
Simanjiro wanakabiliwa na njaa kwani wengi wao wanauwezo wa kununua
chakula.
"Siamini kama Simanjiro wana njaa kwani wana ng'ombe wengi
na ng'ombe mmoja anauzwa hadi sh.500,000 hivyo watumie mifugo yao ili
iwasaidie na siyo kudai kwamba wana njaa ya chakula," alisema Mbwilo.
Alisema
wafugaji wengi hawajapewa elimu ya kutosha juu ya ufugaji wenye tija
ndiyo sababu wanakuwa na mifugo mingi isiyokuwa na faida kwao, kwani
wana uwezo wa kununua chakula na siyo kulalamikia njaa.
Chanzo;Majira
0 comments:
Post a Comment