Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
MKUU wa Wilaya (DC) ya Hanang’, Christine Mndeme, ameombwa
kuingilia kati suala la wananchi wa Kata ya Endasak kugoma kuchangia
ujenzi wa maabara katika shule ya sekondari ya kata yao.
Akichangia mada kuhusu elimu katika kikao cha Baraza la Madiwani wa
halmashauri ya wilaya hiyo, Diwani wa Viti Maalumu, Dainesi Hosea
(CCM), alieleza wananchi wamekuwa kikwazo katika kuendeleza ujenzi huo
kwa kukataa kuchangia wakidai hawaoni faida ya ujenzi huo.
Mkuu huyo wa wilaya, alibainisha suala la wananchi kuchangia elimu
halina ubishi na kumtaka diwani huyo kuwahamasisha na kuwapa elimu ya
kutosha wananchi wake kuchangia ujenzi huo kabla ya ofisi ya mkurugenzi
haijafika katika eneo lake.
“Ile nguvu tuliyoonyesha wakati wa kuchangia ujenzi wa shule za kata
na tuzitumie katika kujenga maabara katika shule hizo, hivyo basi wewe
diwani uende ukawahamasishe wananchi wako wachangie kabla mkurugenzi
hajafika kuhamasisha wananchi hao,” alisisitiza mkuu huyo wa wilaya.
Hata hivyo, Mndeme alisema suala la Shule ya Sekondari Sirop ni la
kusikitisha hasa kwa kuwa na elimu duni inayochangia shule hiyo kufeli
kila mwaka na kuahidi kuifanyia mabadiliko kwa kushirikiana na wananchi
na madiwani wa wilaya hiyo.
Chanzo:Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment