Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Katesh
wilayani Hanang ambapo aliwaambia wananchi wanapaswa kushirikiana na
serikali yao katika kuleta maendeleo na kuachana na mambo mengi
yanayoendelea kwenye siasa.
Katibu
wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Katesh kwenye
mkutano wa hadhara uliofanyika mjini hapo ambapo aliwaambia wananchi
CCM imejipanga vizuri sana kiasi cha wananchi wengi kuendelea kuiamini
,alisisitiza nchi nzima ofisi za CCM zinajengwa na wanachama wake wakati
wapinzani ofisi zao ni za mifukoni.
Mbunge
wa Jimbo la Hanang Mama Mary Nagu akihutubia wananchi wa Katesh ambapo
pamoja na kueleza mipango ya maendeleo pia alitoa mizinga ya nyuki kwa
vikundi vya ujasiriamali.
Mabinti wa Kibarbeig wakifuatilia mkutano wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana mjini Katesh.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Endasak ambao
aliwaambia migogoro mingi waliokuwa nayo ni kwa sababu ya kuhusisha
kila jambo na siasa,miradi inakataliwa kwa sababu za kisiasa hivyo
waweke siasa pembeni wafanye maendeleo.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga mpira kuashiria
kuzinduliwa kwa mashindano ya mpira wa miguu ya CCM Cup Endasak,
Golikipa aliyekuwa golini wakati mpira unapigwa ni Mbunge wa Jimbo la
Hanang Mama Mary Nagu.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ,Mbunge wa Jimbo la Hanang Mary
Nagu,Waziri Mkuu Mstaafu Ndugu Fredrick Sumaye na Mkuu wa Wilaya ya
Hanang Christina Mndeme wakishiriki pamoja na wananchi ujenzi wa ofisi
ya CCM Tawi la Qaloda.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Basoutu na
kuwaambia wachague Viongozi wa kijiji watakaosaidia kuleta maendeleo na
si viongozi watakaorudisha nyuma maendeleo na kuwasababishia migongano
mikubwa kama ya ardhi inayoendelea sasa.
Katibu
Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na Waziri Mkuu Mstaafu
Ndugu Fredrick Sumaye baada ya kumaliza mkutano na wanakijiji ambao
wanamgogoro wa ardhi wilayani Hanang.
0 comments:
Post a Comment