Na Bertha Mollel -Manyara
Warembo wapatao 14 kutoka
vitongoji mbalimbali vya mkoa wa Manyara wameingia kambini mapema jana kwa
lengo la kujifua kwa maandalizi ya kinyang’anyiro cha kumsaka mlimbwende wa
mkoa huo unaotarajiwa kufanyika tarehe 14 katika ukumbi wa CCM hall iliyoko
wilayani Babati.
Akizungumza na Tanzania daima, mratibu wa mashindano hayo Akon Clement kupitia
kampuni ya mererani Entartainment aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Happy Wilium, Edna Mushi, Merry Ruta,
Rose Evason, Flora Godlizen, Amina Omary, Catherine Emmanuel, Sabrina Anger, Bertha Fredrick na
Samila.
Alisema kuwa warembo hao ni kutoka katika vitongoji vya babati, simanjiro na mbulu ambao wameingia rasmi
kambini mapema ili kuweza kupatiwa
elimu na mazoezi juu ya kinyang’anyiro
hicho hasa hasa ikiwemo kuwajengea uwezo
wa kujiamini na kujithamini.
Alisema kuwa shindano hilo la kumsaka malkia wa Mkoa wa Manyara
litasindikizwa na burudani kutoka kwa
wasanii mbalimbali wa mkoa wa Manyara na msanii maalumu kutoka jijini Dar-
es- salaam Bob Junior akipiga hatua kwa
hatua kushusha nyimbo zake mbalimbali
zilizobamba kwenye vyomba vya habari.
Akon alisema kuwa Shindano hilo la
aina yake mjini Babati limedhaminiwa na makampuni mbalimbalia wakiwemo kampuni
ya TBL kupitia kinywaji chake cha Redd’s original, Kifaru
Agrovet, Winners Hotel, wadhamini
wengine ni Active classic Fashion, Open University, kimweri sport wear, Manyara
Computer pamoja na Sarafina Lodge.
“Mimi niseme tu kuwa kwa maandalizi tuliyoyafanya na burudani mbalimbali
tulizoziandaa, niwatonye tu mashabiki na wadau wa urembo na burudani wa mkoa wa
Manyara kuwa watafurahi na kuburudika vya kutosha na hivyo waj itokeze kwa wingi bila kukosa katika kinyang’anyiro
hicho
0 comments:
Post a Comment