Home » » HOSPITALI YA SERENGETI YAKABIDHIWA MTAMBO WA MILIONI 35/-

HOSPITALI YA SERENGETI YAKABIDHIWA MTAMBO WA MILIONI 35/-

Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399. 

 
Hospitali ya wilaya ya Serengeti iliyoko katika mji wa Mugumu imekabidhiwa msaada wa mtambo maalumu wa kupumulia wagonjwa wenye hali mbaya yenye thamani ya Sh. milioni 35.
Msaada huo umekabidhiwa jana na Naibu Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Stephen Kebwe, katika hafla fupi iliyofanyika hospitalini hapo. Dk. Kebwe ambaye pia ni mbunge wa jimbo la Serengeti,  alisema kuwa kifaa hicho amekipata kutoka kwa marafiki zake nchini Marekani na kwamba kitasaidia wagonjwa wenye hali mbaya kupumua vizuri, wakiwa wanendelea na matibabu.

Akipokea msaada huo, Mganga mkuu wa wilaya ya Serengeti, Dk. Salum Manyata ambaye alimkabidhi Mganga mkuu wa hospitali ya Nyerere DDH, Dk. Calvin Mwasha, amemshukuru Naibu waziri huyo kwa msaada huo ambao utasaidia kuhudumia wagonjwa wenye hali mbaya.

Wakati huo huo Dk. Kebwe juzi ameanza ziara katika jimbo lake akiangalia miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo aliyochangia kama mbunge wa jimbo hilo, ambayo yote thamani yake ni zaidi ya Sh. milioni 189.
SOURCE: NIPASHE

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa