THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone: 255-22-2114512, 2116898
E-mail: ikulucommpress@googlemail.com
Website : www.ikulu.go.tz
Fax: 255-22-2113425 |
PRESIDENT’S OFFICE,
STATE HOUSE,
1 BARACK OBAMA ROAD,
11400 DAR ES SALAAM.
Tanzania.
|
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Taratibu za Tiba za Rais zakamilika.
Taratibu
za matibabu ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa
Jakaya Mrisho Kikwete, zimekamilika leo, Jumatatu, Novemba 24, 2014.
Taratibu
hizo za matibabu za Mheshimiwa Rais Kikwete zimekamilika kiasi cha saa
12 asubuhi ya leo wakati madaktari bingwa katika Hospitali ya Johns
Hopkins iliyoko mjini Baltimore, Jimbo la Maryland, Marekani,
walipomfanyia hatua ya mwisho ya tiba.
Hata
hivyo, Rais Kikwete ataendelea kupumzika na kuangaliwa kwenye Hoteli
Maalum inayohusiana na Hospitali ya Johns Hopkins kwa siku mbili hadi
tatu kabla ya kuanza safari ya kurejea nyumbani.
Kama kila kitu kitakwenda kama ilivyopangwa na madaktari, Rais Kikwete anatarajiwa kurejea nyumbani Jumamosi, Novemba 29, 2014.
Rais
Kikwete aliondoka nchini Alhamisi ya Novemba 6, 2014, kwenda kufanyiwa
uchunguzi wa afya yake lakini madaktari katika Hospitali ya Johns
Hopkins waliamua kumfanyia upasuaji wa tezi dume Jumamosi ya Novemba 8,
2014.
Rais
Kikwete anaendelea kuwashukuru Watanzania kwa sala na maombi yao ya
kumtakia heri ya kupona haraka na kurejesha afya njema katika kipindi
chote cha ugonjwa wake.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu – Dar es Salaam.Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment