MKUU wa Wilaya ya Babati Mkoani Manyara, Khalid Mandia amekemea tabia ya baadhi ya watu wanaochochea migogoro kwa wananchi kwa kutumia itikadi za kisiasa, imani za kidini na ukabila.
Alisema hayo jana akiwa katika Kijiji cha Malangi Kata ya Maisaka Halmashauri ya Mji wa Babati. Alisema tatizo hilo ni changamoto kubwa kwa Taifa na kuharibu usalama wa nchi, na ukosefu wa uaminifu miongoni mwa watendaji.
Alisema katika miaka ya hivi karibuni, limejitokeza wimbi la baadhi ya viongozi na wananchi wachache kuwa na hulka ya kujilimbikizia mali au utajiri, ambao umekuwa ukitafutwa kwa njia mbalimbali, zikiwemo za rushwa na zisizo za halali.
“Tushirikiane kubainisha aina hii ya uhalifu ili kila mmoja wetu aishi kwa kutumia njia halali, kwani ubaya haulipi, na pia kisasi kimoja huzaa kisasi kingine kikubwa zaidi na hatimaye kuchochea machafuko,” alisema Mandia.
Alitaka wananchi kujitokeza kwa wingi, kuwachagua viongozi wa ngazi za mitaa. Alitaka vyama vyote vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi huo, kuhakikisha uchaguzi huo unakuwa wa amani na utulivu.
Chanzo;Habari Leo
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment