Mkuu wa mkoa wa Manyara ,Mhe.Joel Nkaya Bendera akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa huo kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati,kushoto ni Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi na kulia ni Mkuu wa wilaya ya Babati,Crispin Meela.Mhe.Bendera amesisitiza nidhamu ya kazi katika kuhudumia wananchi na ameapa kuwaondoa watendaji wabovu mkoani humo.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza katika kikao cha viongozi wa wilaya zote za mkoa wa Manyara kilichofanyika ofisi ya Mkuu wa Mkoa mjini Babati.Ameuagiza uongozi wa mkoa huo kumaliza migogoro ya ardhi ifikapo mwezi Mei mwaka huu.
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakimsikiliza Waziri wa Ardhi(hayupo pichani)alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
Wananchi wa mkoa wa Manyara wakipeana maelekezo yaliyotolewa na Waziri wa Ardhi ya namna ya kuwasilisha malalamiko yao kwa maandishi alipokutana nao kusikiliza kero za migogoro ya ardhi inayosababishwa na watendaji wa sekta hiyo kwenye ukumbi wa halmashauri ya wilaya ya Babati.
Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Lukuvi akizungumza na wananchi wa mji wa Babati waliojitokeza kuwasilisha kero zao zinahusu migogoro ya ardhi.Kikao hicho kilihudhuriwa pia na wabunge wa mkoa wa Manyara.
Katibu Tawala wa mkoa wa Manyara,Mhandisi Omar Chambo akisoma taarifa ya migogoro ya ardhi mkoani humo kwa Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi,Mhe.William Vangimembe Lukuvi kwenye ziara yake ya kusikiliza kero za ardhi.
Ikiwa unatukio lolote au jambo lolote tuma kupitia Barua pepe yetu blogzamikoa@live.com au Whatsapp namba +255765056399.
0 comments:
Post a Comment