Wananchi
wa Mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, wakitoa
kero kwa Mkuu wa Mkoa huo Alexander Pastory Mnyeti.
Mkuu wa Mkoa wa Manyara Alexander Pastory Mnyeti akizungumza na wananchi wa mji mdogo wa Orkesumet Wilayani Simanjiro.
MKUU
wa Mkoa wa Manyara, Alexander Pastory Mnyeti amewataka mahakimu wa mkoa
huo kutekeleza wajibu wao ipasavyo wakati wanaposikiliza kesi na kutoa
hukumu kwa haki ili kuepuka malalamiko yanayotolewa na wananchi.
Akizungumza
kwenye ziara yake ya kwanza ya siku saba katika Wilaya ya Simanjiro,
Mnyeti alisema kupitia nafasi yake ya Mwenyekiti wa kamati ya maadili,
hatakubali kuona wananchi wanalalamikia kukosa haki.
Mnyeti
alisema baadhi ya mahakimu wanajigeuza kuwa miungu watu na kushindwa
kutekeleza wajibu wao ipasavyo hivyo kusababisha malalamiko kwa
wananchi. "Hatuwezi kukubali kuona mambo kama hayo,
yakifanyika kama kuna mtu anaona kuna mahakimu siyo waadilifu wanakula
rushwa na kushindwa kutoa haki nijulisheni," alisema Mnyeti.
Awali, mkazi wa mtaa wa Njiro, Theopista Paulo alisema amekuwa akinyanyasika wakati akidai haki yake. Theopista
alisema mmoja kati ya mahakimu wa eneo hilo alikuwa anamwambia hata
kama akimkataa na kesi yake kuhamishwa kwenye mahakama nyingine hawezi
kushinda chochote.
Hata
hivyo, Mwanasheria wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo, Peter Mangala alisema
mwananchi yeyote ana haki ya kumkataa hakimu endapo atakuwa na sababu za
msingi. Mangala alisema endapo mwananchi akiwa na hoja za
msingi anazozipinga anaweza kumkataa jaji au Hakimu atakapobaini kuwa
hawezi kutendewa haki.
0 comments:
Post a Comment