Home » » LEO TUNAANGAZIA KWA UFUPI SEKTA YA MALIASILI KATIKA WILAYA YA KITETO MKOANI MANYARA

LEO TUNAANGAZIA KWA UFUPI SEKTA YA MALIASILI KATIKA WILAYA YA KITETO MKOANI MANYARA


MALIASILI
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto na misitu ya hifadhi Ha.548696.13. Kati ya misitu hiyo Ha. 466.6 ni ya Serikali Kuu ambayo ni asilimia 0.1. Misitu ya hifadhi inayomilikiwa na jamii ni Ha.548,129.53.
Sekta hii ya Maliasili inahusika na sekta ndogo za misitu, nyuki, wanyamapori, uvuvi na Utalii. Sekta hii inajihusisha na usimamizi wa rasilimali za Maliasili na kuhakikisha matumizi endelevu ya Maliasili hizo kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo.
Katika shughuli zinazofanywa katika kuhakiakisha kuwa maliasili na mazingira yanatunzwa vizuri halmashauri inahimiza upandaji wa miti ambapo lengo la upandaji miti katika mwaka 2007/2008 lilikuwa ni kupanda miti 1,500,000. Hadi kufikia Jan.2008 jumla ya miti 503000 ilioteshwa na upandaji wa miti hiyo unaendelea sambamba na upandaji wa miti ya (maotea, Vigingi (Cuttings) na mbegu ) (tick)ili kufikia lengo lililowekwa.
Mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu (PFM):
Halmashauri ya Wilaya ya Kiteto kwa mwaka wa fedha 2007/2008 ilijieweka malego ya kuendelea na utekelezaji wa Mpango wa Usimamizi Shirikishi wa Misitu (PFM) katika vijiji 5 ambapo jumla ya Shilingi 110,403,055 zilitengwa.
Shughuli zilizohusika ni pamoja na na Usimamizi shirikishi wa misitu ya hifadhi ya Serikali kuu na Halmashauri ya Wilaya, Uanzishaji wa misitu ya hifadhi kwenye ardhi za vijiji, Kusaidia uanzishaji wa shughuli za kiuchumi katika vijiji husika na Kujenga uwezo kwa watumishi wa ngazi ya Halmashauri na kamati za mazingira za vijiji.

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa