Home » » Polisi wajinoa

Polisi wajinoa


na Said Kopwe, Manyara
KATIKA kuhakikisha nchi inaendelea kudumisha amani na utulivu, Jeshi la Polisi limeendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo askari wake kukabiliana na changamoto za ulinzi wa raia na mali zao.
Mafunzo hayo, yameanza kutolewa hivi karibuni, baada ya kufunguliwa na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Akili Mpwapwa.
Katika muendelezo wa mafunzo hayo, mwishoni mwa wiki, yaliendeshwa mafunzo ya utayari kwa askari wa wilaya zote pamoja na askari wa vikosi vyote vya Mkoa wa Manyara.
Baada ya ufunguzi huo, baadaye Mkuu wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) Mkoa wa Manyara, akiambatana na Mkuu wa Operesheni Mkoa, Inspekta Genes, pamoja na walimu wawili askari namba F. 9853 PC Jumanne na G. 225 PC Joshua, kwa pamoja walitoa mafunzo hayo kwa askari wa wilaya zote.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa