Picha ikimuonyesha mwenyekiti wa kijiji cha Rkeepusi Bw.Tung’ungwa Leyaan akiwa anaelezea juu ya tatizo la chakula inayowapelekea wamasai kuhamia mijini
Imeelezwa kuwa Halisi si swari Wilaya ya Ngorongoro kutokana na ukosefu mkubwa wa chakula hali inayopelekea wananchi hao wa jamii ya wafugaji kuhama makazi kutokana na ukosefu huo wa chakula
Pia wananchi hao wameitaka serikali kuwarudishia kilimo chao cha viazi ambacho awali walikuwa wanalima katika eneo hilo la tarafa ya ngorongoro ili waweze kujikimu katika suala la chakula badala ya kutegemea serikali na chakula chake cha msaada
Wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro ambao ni jamii ya wafugaji(wamasaai)wameonyesha kukerwa na hali hiyo huku wakiitaka serikali kuchukua hatua za haraka ili kuwanusuru jamii hiyo na janga la njaa
Akiongea na blog hii ya jamii mwenyekiti wa kijiji cha Rkeepusi Bw.Tung’ungwa Leyaan alisema kuwa kwa sasa wananchi wamekuwa na hali mbaya sana ya ukosefu wa chakula jambo ambalo linawapelekea wao kuhama makazi yao na kuja mijini kutafuta ajira huku ajira nyingine zikiwa si rasmi
“Wamasaai sasahivi wamekuwa wengi sana hapa mijini kutokana na ukosefu wa chakula na kama mtu yeyote ana njaa hawezi kukaa lazima atafute sehemu yenye chakula ili aweze kula nah ii sasa inapelekea wao kuwa walinzi katika majumba ya watu n.k”
Akielezea kwa uchungu juu ya suala la njaa alisema kuwa tatizo hilo ni kubwa na ukizingatia kuwa hawalimi imekuwa tatizo kubwa sana kwao kwa kutegemea tu ufugaji
“Miaka ya nyuma tulikuwa na kilimo cha kujikimu cha kukima viazi na baadae kuja kusitishwa na serikali kwa madai kuwa hiyo ni sehemu ya hifadhi’alisema
Mwenyekiti akiwa na mwenzake akiwaanaelezea kwa kina juu ya tatizo hilo
Katika hilo alihoji serikali iwapo itaweza kuwahudumia kwa chakula cha bure hadi lini huku akisema kuwa hata kama mtu anakupa msaada flani mara kwa mara itafiakia mahali atachoka kutoa msaada huo
Chanzo: Pamela Mollel blog
0 comments:
Post a Comment