Home » » WACHIMBJI WATAKA WAAJIRI KUIPA KIPAUMBELE HUDUMA YA AFYA

WACHIMBJI WATAKA WAAJIRI KUIPA KIPAUMBELE HUDUMA YA AFYA


na Mwandishi wetu, Simanjiro-Manyara
WACHIMBAJI wadogo wa madini Mkoa wa Manyara, wilayani Simanjiro,wamezitaka kampuni na sekta binafsi zinazojishughulisha na uchimbaji madini nchini, kuangalia namna ya kutatua tatizo la huduma ya afya linalowakabili.
Kauli hiyo imekuja kufuatia kampuni na sekta hizo kutothamini afya za wafanyakazi wake wakati wakiwa migodini, hali inayowasababishia wengi wao kukosa imani kwa waajiri wao.
Akizungumza na Tanzania Daima kutoka Simanjiro jana, mmoja wa wachimbaji hao, Othuman Rashidi alieleza kusikitishwa kwa uzoroteshaji wa huduma hiyo kwenye kampuni na sekta hizo, licha ya kuwa miongoni mwa wafanyakazi wanaokabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo ya mshahara mdogo.
Aidha, alisema mbali na ufinyu wa huduma hiyo kwa wafanyakazi wanapofikwa na maradhi, lakini bado hawathaminiwi kama wafanyakazi wengine katika kampuni au sekta ukilinganisha na mazingira hatarishi wanayofanyia kazi.
“Unajua tunazungumzia suala la mfanyakazi akiugua wakati tupo huku mgodini, mosi hewa hafifu, huduma ya afya hamna hadi tupande juu, na hapa kuna kampuni zenye mashine ya kupanda na kushuka na nyingine hazina, hivyo inatulazimu kumbeba mgonjwa huku tukipanda kwa miguu kwenda juu kwa ajili ya kumtafutia huduma ya kwanza, kikubwa hili ni tatizo kwetu,” alifafanua Rashidi.
Chanzo: Tanzania Daima

0 comments:

 
Supported by Tone Multimedia Company Limited
Copyright © 2012. Manyara Yetu - All Rights Reserved
Designed by Fredy Tony Njeje
Proudly powered by Blogs za mikoa