WILAYA za Nzega-Tabora, Mbulu-Manyara na
Iramba mkoani Singida zimeanza mchakato wa kuunda timu ya wataamu kwa ajili ya
kuielimisha jamii katika maeneo yao juu afya na usafi wa mazingira.
Hatua hiyo imekuja
baada ya kufanyika kwa mradi wa majaribio katika kata tatu za Wilaya hizo
na kuonesha mafanikio makubwa, huku katika maeneo mengine tafiti zikionesha
kuwa zaidi ya asilimia 50 ya kaya hazina vyoo vinavyokubalika kiafya hali
inayosababisha magonjwa ya mlipuko.
Meneja wa Shirika la
SEMA-Singida bwana Ivo Manyaku moja ya asasi zilizowakusanya wadau hao
mjini Kiomboi Singida kwa siku tano, amesema lengo ni kupata timu ya wataalamu
wa kuelimisha jamii na kuhamasisha juu ya afya na usafi wa mazingira
vijijini ili kupunguza magonjwa.
Mgeni rasmi katika ufunguzi
wa mafunzo hayo mkurugenzi mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Iramba
Bibi Halima Mpita anasema usafi wa mazingira ni muhimu katika kulinda afya za
wananchi.
Mpango huo wa
kuunda timu ya wahamasishaji na waelimishaji jamii juu ya afya na usafi wa
mazingira, umekuja baada ya kufanyika kwa mradi wa majaribidiio katika kata
za Mambali-Nzega, Masieda-Mbulu na Mtoa Iramba ambapo kiwango cha
ujenzi wa vyoo bora kimefikia zaidi ya asilimia 80.
0 comments:
Post a Comment