Kiteto. Mapigano baina ya wakulima na wafugaji
wilayani Kiteto Mkoa wa Manyara yameibuka tena na kusababisha mtu mmoja
kuuawa kwa kukatwa kichwa katika Kijiji cha Kondevesi.
Tukio hilo ni la pili ndani ya wiki moja, ambapo
awali watu wawili waliuawa na wengine nane kujeruhiwa katika ugomvi wa
aina hiyo. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Manyara, Akili Mpwapwa
alithibitisha kuuawa mfugaji huyo.
“Ni kweli kuna mfugaji wa kimasai ameua, jina lake
halijatambuliwa na msako wa kuwakamata waliohusika umeanza,” alisema
Mpwapwa. “Ni mapigano ya kulipiza kisasi baada ya awali wakulima
kuwashambulia wafugaji wakulima na kuamua na kujeruhi,” aliongeza
Mpwapwa.
Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya ya
Kiteto, Dk Thomas Ndalio alisema hali za majeruhi saba kati ya wanane
waliolazwa katika hospitali hiyo zinaendea vizuri.
DK Ndalio alisema majeruhi mmoja, Musa Juma hali yake ni mbaya na aliwahishwa Hospitali ya Mkoa wa Dodoma.
Aliwataja majeruhi waliokatwa kwa sime, mikuki na
visu kuwa ni mtoto wa miaka 12, Juma Bahati, Emmanuel Mathias (26), Hoti
Damiani (38), Mwajuma Hamis (20).
Wengine ni Habiba Ally (16) na Mwajuma Martin (33) ambao wote bado wanapewa matibabu.
Dk Ndalio alisema katika mapigano hayo yaliyotokea
Desemba 21 mwaka, huu alipokea miili ya watu wawili waliouawa katika
eneo la mapigano Kijiji cha Olpopong wilayani humo.
Chanzo;Mwananchi
Chanzo;Mwananchi
0 comments:
Post a Comment