JESHI la Polisi mkoani Manyara linaendelea na msako katika wilaya
zake, hasa maeneo ya vijijini kwa lengo la kudhibiti na kukomesha
uhalifu hasa katika kipindi hiki cha kuelekea sikukuku za mwisho wa
mwaka.
Kaimu Kamanda wa Polisi mkoani Manyara, Mussa Marambo, alisema jana
kuwa katika msako uliofanyika katika vijiji vya Olasiti na Vilima kwa
siku tano, walifanikiwa kuwakamata watuhumiwa wawili waliodaiwa kukutwa
na mirungi na mtuhumiwa mwingine alitoroka.
Alisema mtuhumiwa Tumaini Mrema alikamatwa katika Kitongoji cha Mdori
akiwa na kilogramu tano za mirungi ndani ya basi la Ntoku lenye namba T
342 BXN, lililokuwa likitokea Arusha kuelekea Singida.
Marambo alisema mtuhumiwa mwingine, Mussa Kamari ambaye ni dereva wa
basi la Kampuni ya Mohamed Classic lenye namba T 163 AJR linalofanya
safari zake Arusha na Mwanza, alikamatwa na kilogramu 10 za mirungi
katika Kijiji cha Olasiti.
Alimtaja mtuhumiwa aliyetoroka kuwa ni Sawa Maliki, mkazi wa Kijiji
cha Vilima Vitatu na kusema kuwa alikutwa na pombe aina ya gongo lita
40 pamoja na mtambo wa kutengenezea pombe hiyo. Polisi wanaendelea
kumsaka
Chanzo;Tanzania Daima
0 comments:
Post a Comment